» » » Hawa Ndio Wasanii 10 wenye Pesa zaidi Africa

Channel O ya south Africa imeshiriana na Forbes na kutoa orodha ya wasanii 10 wa Afrika wenye Mkwanja zaidi. List hii imekuwa compiled kwa kuzingatia vigezo hivi:- Sales, Social -Media presence, endorsement value, YouTube views, show rates , Influence, appearance in newspapers, investments, popularity and other factors.Tuanze Countdown yetu.


10. Banky W (Nigeria)

Olubankole Wellington au unaweza kumuita Banky W alizaliwa  March mwaka 1981 huko nchini marekani. Banky W ni mwanamuziki anayeimba miondoko ya RnB nchini Nigeria na watu wengi wamekuwa wakimuita mfalme wa Rnb kwa upande wa Afrika. Banky. Kipaji chake cha Muziki na Uwezo wake wa kufanya mikataba ya kibiashara ndio imemfanya moja kati ya wanamuziki matajiri kabisa Afrika. Ameshakua Brand ambassador wa Etisalat Nigeria na sasa anaonekana kwenye matangazo mbalimbali ya Bidhaa za Samsung. Banky W pia ana Mr capable foundation ambayo kazi yake ni kusaidia kutoa elimu kwa watoto wanaotoka kwenye familia masikini.
09 . Ice Prince (Nigeria)
Panshak Zamani au unaweza kumuita ice prince ni msanii mwingine kutoka Nigeria aliyeingia kwenye list hii.Alizaliwa October 30 mwaka 1986. Ice Prince ni  mshindi wa 2013 BET Awards  kwenye category ya  “Best International Act Africa”. Vitu vinavyomuingizia pesa ni Muziki akiwa na 6 million downloads so far, Akimiliki Studio 2 , pia ni ambassador wa Plug n Play.
08. Sarkodie (Ghana)
Sarkodie ni Rapa kutoka Nchini ghana.Anamilikini Clothing line inayoitwa Sark Clothing pia ni ambassador wa  Samsung and Fan Milk nchini  Ghana.
07. Anselmo Ralph (Angola)
Anajulikana sana kama Prince wa angola.Anselmo ni muimbaji wa miondoko ya Rnb / Soul nchini Angola.anamiliki Perfumes zake mwenyewe, ana clothing line, tour businayogharimu mamilioni ya shillingi. Ukiachana na hayo Anselmo ni Ambassador waSamsung na Cocacola.Anselmo yupo chini ya label ya Sony Music.
06 . 2 Face Idibia (Nigeria)
Najua wengi mnamjua 2 Face Idibia. Huyu ni Singer , Song writer na producer kwa pamoja. @2face ametengeneza 10 million discs na anamauzo ya mtandao yasiyopungua 7 million. 2 Face ni UN ambassador for youth and peace.Anamikataba ya biashara na  Guinness, Haven Homes, na Airtel Worldwide . Pia ana organization yake inayoitwa  Tuface Idibia Foundation.
05. WIZKID (Nigeria)
Ayodeji Ibrahim Balogun au unaweza kumuita Wizkid amezaliwa July 16 mwaka 1990. Yupo chini ya label ya EME akiwa na ushirikiano na Disturbing London. Ameshafanya international Collaboration na Wale , Ameimba na Chris Brown on Stage twice. Wiz Kid ndiyo Pepsi Ambassador anayechukua mkwanja mkubwa zaidi compared to others. Pia wizkid ni ambassador wa mtandano wa MTN.
04. D’Banj (Nigeria)
Dapo Daniel Oyebanjo  a.k.a D’Banj azaliwa June 9, 1980.Ana awards kibao kama  MTV Europe Music Awards for Best African Act 2007, MTV Africa Music Awards2009 Artist of the Year. BET Awards of 2011 for Best International Act Africa. Ni CEO wa DB Records .Anamiliki  koko Lounges;club maarufu nchini Nigeria pia  Koko Water.D banj alipata   million 1 za kimarekani kwa ajili ya kutengeneza reality show yake mwenyewe inayoitwa  Koko Mansion. D’banj anamiliki crib jijini  Atlanta , Marekani lenye thamani ya  1.5 million Dollars .
03 . P-Sqare (Nigeria)
Nigerian R&B duo Peter and Paul Okoye ni kati ya wanamuziki matajiri kabisa  Africa.Wanaproduce muziki wao kupitia Studio yao ya Square Records. Mwezi December 2011, walijoin music label ya  Akon’s Konvict Muzikna baadae walisign na Universal Music South Africa kwa ajili ya usambazaji wa kazi zao. Kwasasa ukitaka P-Square waje kukupigia show inabidi utoe pesa isiyopungua  150,000 US Dollars  per show. Square ville ndio jina la crib yao iliyopo  Ikeja yenye thamani ya  3 million USD . Pia P-sqaure wana mkataba wa miaka mitatu na  Globacom , kampuni ya mawasiliano nchini Nigeria  as brand ambassadors ambapo wanalipwa mamilioni ya dollars kwa mwaka.
02. Don Jazzy (Nigeria)
Don Jazzy ni CEO wa  MAVIN records aliyoianzisha mwezi  May, 2012 baada ya kutengana na rafiki wake wa utotoni na music hit  partner, D’banj. Ukiachana na yeye kuwa music producer na Song Writer , Don Jazzy pia ni Multi-Award Winning musician na mjasiriamali. Don Jazzy ni Brand Ambassador wa Samsung, Loya Milk na MTN. Ameshafanya kazi ya music production na watu kama D’Banj, Kanye West, Beyonce na American Rapper Jay Z.

don-jazzy
01. Akon (Senegal)
 Kuna wengi ambao mnashangaa kwanini Akon yupo katika hii list lakini ukweli ni kwamba Akon bado ni Mtu Afrika na ni raia wa nchi ya Senegal. Akon alianza kujulikana mwaka  2004 baada ya kuachia ngoma ya  “Locked Up”, ambayo ndio ilikua nyimbo ya kwanza kwenye album yake ya  Trouble. Akon ndio Solo Artist wa kwanza kushikilia nafasi ya kwanza na ya pili mara mbili kwenye chart za billboard.Akon ana utajiri unaokadiriwa Dola za kimarekani millioni 80.


Tunaomba Maoni yako Hapa :

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply