Jana mtandao wa Globalpublishers ulitoa habari ukimnukuu Irene Uwoya akisema kuwa muigizaji mwenzake Lucy Komba ana lengo la kumzunguka na kumharibia ndoa yake sababu ikiwa ni Lucy Komba kucheza filamu pamoja (Kwanini Nisimuoe) na Hamad Ndikumana raia wa Rwanda ambaye alimuoa Irene Uwoya na mara kwa mara magazeti na mitandao kuripoti kuwa wametengena ingawa haijadhibitika rasmi mpaka sasa kama ni kweli wametengana sababu kubwa ikidaiwa ni skendo za mara kwa mara za Uwoya zinazoripotiwa magazetini.
Baada ya habari hizo kuenea kwenye mitandao jana Swahiliworldplanet iliamua kuzungumza na Lucy Komba kutokea nchini Denmark alipo sasa ili kupata maoni ya upande wake baada ya habari hiyo. Kwanza Lucy alionekana kama kushangazwa na kauli ya Uwoya halafu alicheka na kusema kuwa hata yeye yupo nje ya nchi kama Uwoya ambaye yupo Swazland kwasasa hivyo hawezi zungumzia suala hilo mpaka atakaporudi nchini ndiyo atazungumzia suala hilo "Ha ha nimesoma Siwezi kuongea chochote kuhusu Hilo kwani hata mimi sipo Tanzania nikirudi ndo nitaliongelea hilo" alisema Lucy Komba ambaye ndiye aliyemuingiza Uwoya kwenye filamu akitokea kwenye umiss.
Hata hivyo historia inaonyesha kuwa Lucy Komba ameibua vipaji vingi vya filamu nchini kutoka katika kada mbalimbali kama vile muziki, mitindo na hata waigizaji wengine chipukizi wasiotokea katika fani nyingine kwa kuwapa nafasi ya kucheza katika filamu zake mbalimbali akiwemo Uwoya mwenyewe hivyo hatudhani kuwa ni tatizo kama ameona kipaji cha Ndiku na kuamua kukiendeleza. Nakuhusu madai ya Irene kuwa Lucy hakumueleza kuhusu kucheza filamu na mumewe hili linaweza kuwa jukumu la Ndiku mwenyewe kwani ni mtu mzima na kama mume. Na kama kweli amekuja nchini na kucheza filamu bila kumwambia Irene wala kumshirikisha ni lazima kutakuwa na walakini kwa wanandoa hao maana ni jambo lisilowezekana mume atoke nchi nyingine na kuja nchi anakokaa mkewe bila kuonana tena akifanya kazi kubwa ya filamu ambayo mwisho wa siku ni lazima iwe hadharani kwa mashabiki(public) akiwemo mkewe kuitazama.
Ukiachilia hayo hapo juu baadhi ya watu wakiwemo wasanii wawili waliokataa kutajwa majina yao walituma ujumbe SWP baada ya kusoma habari hiyo na kusema.....
Msanii 1: "ha ha ha haaaa, Uwoya asijifarague kwa kutafuta pa kufichia aibu yake, alishampa stress mwanaume wa watu kwa kujitia star mara kibao, alishaharibu ndoa yake tangu siku nyingi mbona !"
msanii 2: Looh.... haya makubwaaa! amesahau ya hivi karibuni tu kwa Diamondoooo......! shauri yake wenzake wanataka ndoa ye anaichezea, na kama Ndiku ni kweli anatoka na Lucy basi kaona anamfaa.
Katika mitandao mbalimbali iliyoweka habari hiyo jana baadhi ya maoni ya watu ni hayo hapo chini.......
Dosca Kusenha: aache uhuni mbona yeye aliduu na Diamond...amuache dada etu kwanza hana kawaida ya kula vilivyoliwa
Sam Mdee: kila mla vya wenzie ajue na vyake vtaliwa
Sikitu Husein: Uwoya hana akili mi naonaa .....kama kweli anampenda ndiku na ndoa yake why anatumia jina la Irene wa Ferola ktk Instagram wakat feregola ni jina la mwanaume mwingine wa Congo, y asiandike jina la mumewe ndiku, shame on u Uwoya!!!!
Nyamgomera Muhozi: jamani kumbe mkuki kwa nguruwe kwa binadamu mchungu uwoya amesahau diamond alipomla uroda hotelini anafikiri mmewe huyo hakusikia uchungu?
Anonymous: Uwoya bado anayo haki ya kumlinda mumewe hata kama ameharibu mwenyewe, wasanii wa bongo movie pia hawaaminik, na we uwoya utakuja juta siku moja kwa kumtesa shemej yetu, tulia mwanamke.
Hellen Mathias: mhh..shughuli.
Mseli Msuya: Irene pole, ndio maumivu ya mapenzi hayo! ujue na mumeo naye anapata maumivu kwa njia moja ama nyingine akisikia vibweka vyako kama cha juzi wewe na diamond, kimjini tunasema kuwa mpole ngoma droo.
Mjingamjinga Mzee Ali: mtenda akitendewa upita akilaumu wakati kila ula kuku wa mwezio juwa miguu ukulekea.
Husna Mwalimu: wee uwoya na kule instagram watumia jina la nani vileee! bitch....!!!
Anne Msuya: mtenda akitendewa upita akilaumu wakati kila ula kuku wa mwezio juwa miguu ukulekea.
Schola Temu: Lucy kama Ndiku kakapenda usivunge Uwoya katutia aibu wanawake wa Bongo tunaonekana hatujui kuthamini ndoa. ustar ni kitu cha kupita uwoya lakini mume huleta familia milele. jipange
Massali Imma: Mfamaji haishi kutapatapa umeshachelwa ndugu
Kiliane Kipande: mtenda hutendw ni zamu yako sasa!
Stellah Mapande: Una haki ya kumlinda mumeo lakini ushachelwa...umemtenda Ndiku wa watu mpaka akazimiaa, zamu yako sasa!
Anonymous: Wewe ukimuona wa nini wenzio wanajiuliza watampata lini, namshangaa huyo Irene kujifanya kuhoji wakati mwanamme kamshindwa mwenyewe. Lucy mama ikiwezekana kama ni kweli mnadate chukua chombo kimoja hamna kulegeza uzi. Mwanaume anahitaji kuenziwa bibi yamekushinda waachie wenye meno watafune.
Anonymous: Uwoya alikimbilia ndoa wakati damu yake bado inataka kila mwanaume, ndiku usirudi nyuma funga ndoa kabisa na da Lucy ye anajiheshimu na kama sio kweli kuwa na wapenzi basi tafuta hapahapa Tz utampata mwanamke mzuri anayejua kutunza mume.
HAPA CHINI NI BAADHI YA PICHA KUTOKA FILAMU YA 'KWANINI NISIMUOE' BY LUCY KOMBA AND HAMAD NDIKUMANA.
news via: GPL
No comments: