» » » » The Game aamua kuchoma Jezi ya Dwight Howard.Ni Baada ya Mchehzaji wa timu ya Lakers Dwight Howard Kutosain Mkataba Mpya wa Lakers


San Antonio Spurs v Los Angeles Lakers - Game Three
Nyota wa Hip-Hop anayewakilisha West Coast akitokea huko Compton California Jayceon Taylor ambaye wengi humfahamu kwa jina la jukwaani la The Game amefunguka kuhusu issue nzima ya kuondoka kwa mchezaji Dwight Howard ambaye siku ya ijumaa alifanya maamuzi ya kutosaini mkataba mpya na timu ya Los Angeles Lakers na kuhamia Houston Rockets .
Game ambaye ni shabiki mkubwa wa Los Angeles Lakers aliwashauri mashabiki kutochoma moto jezi namba 12 iliyokuwa na jina la HOWARD kwa kuwa wanaweza kuhatarisha usalama wa nyumba zao kwa kusababisha ajali ya moto . Game amewashauri mashabiki wa Lakers wanaomiliki Jezi ya Howard waikate nusu na kubakia na kipande cha mbele chenye nembo ya Lakers na kutupa upande wa nyuma wenye jina La Howard .

game1
Game amesema kuwa kuondoka kwa Howard sio issue kwa Lakers kwa kuwa timu hiyo ilikuwepo na ilipata mafanikio  kabla Howard hajaja na itaendelea kupata mafanikio maradufu baada ya mchezaji huyo kuondoka hivyo mashabiki hawapaswi kuwa na wasiwasi juu ya kuondoka kwake .
Rapa huyo aliongeza kuwa hawezi kumhukumu Dwight kwa kile alichokifanya kwa kuwa amefanya maamuzi kama mtu mzima na amefanya maamuzi hayo kwa kuifikiria familia yake na kile anachokitaka kama mchezaji na mwanadamu hivyo uamuzi wake unapaswa kuheshimiwa .
Game alitoa kali baada ya kubadilika wakati mahojiano hayo yalipokuwa yanaelekea ukingoni ambapo alisema kuwa pamoja na mazuri yote aliyoyasema ” Bado yeye (Game ) kama Shabiki wa Los Angeles Lakers bado ataichoma moto jezi yake yenye jina la Dwight Howard kwani hajafurahishwa na kitend cha Howard kuisaliti Lakers na kuhamia Houston Rockets.

Tunaomba Maoni yako Hapa :

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply