» » Angel wa ‘Baadaye’ ya Ommy Dimpoz na Tana wa Tanchy waingia kwenye TPF6 academy



Msanii wa kike aliyetajwa mwaka huu kuwania tuzo za Kili kwenye kipengela cha msanii bora anayechipukia, Angel, maarufu kwa kuweka kionjo kwenye wimbo wa Ommy Dimpoz na Tana wa kundi la Tanchy (Tana and Chibwa) ni miongoni mwa wawakilishi wa Tanzania walioingia kwenye Tusker Academy mwaka huu.

Angel akiimba na Ommy Dimpoz kwenye birthday ya Vanessa Mdee, June 8



Tana alizaliwa kwa jina Happy Jaffari Kalinga. Ana pacha wake wa kiume aitwaye Alex Jaffari Kalinga. Anaunda kundi liitwalo Tanchy akiwa na Chibwa ambaye pia ni mpenzi wake. Kabila lake ni mhehe na alizaliwa mwaka 1990 katika hospitali ya Aga khan jijini Dar es Salaam.


Shule ya msingi amesoma St Mary’s mpaka sekondari na kumalizia Happy Skillful Secondary mwaka 2008. Chuo amesema DJS mpaka level ya Diploma. Alianza muziki mwaka 2007 akiwa kidato cha nne.

Washiriki wanne wa Tanzania wameingia kwenye TPF6 Academy.

Tunaomba Maoni yako Hapa :

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply