Unknown
12 years ago
It’s official, Rostam Aziz ndiye bilionea pekee wa Tanzania (kwa dola). Kwenye orodha mpya ya matajiri 50 wa Afrika, Rostam Aziz ameingia kwa mara ya kwanza na kwa kishindo.
Utajiri wake umechangiwa zaidi na kuwa na asilimia 35 ya hisa za kampuni ya Vodacom Tanzania, yenye watumiaji zaidi ya milioni 9.5. Anamiliki kampuni ya Caspian Mining, inayotoa huduma za uchimbaji kwenye migodi mikubwa nchini inayomilikiwa BHP Billiton na Barrick Gold. Utajiri wake unamfanya awe mtu wa pili Afrika Mashariki kuwa bilionea nyuma ya Sudhir Ruparelia wa Uganda na pia kukamata nafasi ya 27 kwenye orodha ya Forbes mwaka huu.
Mwenyekiti Mtendaji wa makampuni ya IPP, Reginald Mengi amemfuata kwa mbali Rostam kwa kuwa na utajiri wa dola milioni 550 na kukamata nafasi ya 34 kwenye orodha hiyo ya Forbes.
Utajiri wa Mengi, ambaye naye ndio ameingia kwa mara ya kwanza kwenye orodha ya matajiri wa Afrika umetokana na kuwa na himaya kubwa ya vyombo vya habari. Anamiliki magazeti 11 yakiwemo Nipashe, Financial Times, ThisDay na The Guardian, vituo vya TV, (EATV, Capital na ITV), Radio One, EA Radio na Capital FM. Mengi pia anamiliki mgodi wa dhahabu pamoja na kiwanda Coca-Cola.
Kwenye nafasi ya 38 wapo Said Salim Bakhresa na Mohammed Dewji wenye utajiri wa dola milioni 500 kila mmoja.
Kwenye orodha hiyo, tajiri wa Nigeria Aliko Dangote anayemiliki kiwanda cha saruji mjini Mtwara ameendelea kukamata namba moja kwa kuwa na utajiri wa zaidi ya dola bilioni 20.
Ingia hapa kuona orodha nzima ya Africa’s 50 Richest.
Tunaomba Maoni yako Hapa :
Category:
Forbes
Related Posts

Hawa Ndio wanawake100 wenye nguvu Dunaini kwa mwaka 2014, Beyonce, Shakira, Lady Gaga waingia kwenye orodha ya mwaka huu 'Forbes'
Jarida Maarufu Duniani la Forbes Jumatano hii limetoa orodha mpya ya wanawake 100 wenye nguvu zaidi ...Read more »
29May2014
Hawa ndio wasanii wa5 Matajiri zaidi wa Hip Hop kwa mwaka 2014
Jarida maarufu la Forbes imetoa orodha ya wasanii wasanii watano wa Hip Hop matajiri zaidi 2014. Sea...Read more »
17Apr2014
Most Overexposed Celebrities in 2014 ni Justin Bieber na Kim Kardashian 'waongoza orodha ya Forbes '
Forbes imetoa orodha ya mwaka ya ‘Most Overexposed Celebrities’, na kwa mwaka huu Justin Bieber ndi...Read more »
13Mar2014
January Makamba na Mohammed Dewji ni miongoni mwa watu 10 wenye nguvu Afrika, 2014 ' Forbes'
Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba pamoja na Mbunge wa Singida Mjin...Read more »
01Feb2014
FORBES : MATAJIRI 50 AFRIKA KWA MWAKA 2013, KUTOKA TANZANIA NI MENGI,ROSTAM,DEWJI
This year, nine individuals join the ranks of Forbes’ third annual ranking of the richest people in ...Read more »
05Dec2013
WANAMUZIKI WALIOINGIZA PESA NYINGI ZAIDI 2013, MODONNA AKAMATA NAFASI YA KWANZA ICHEKI LIST NZIMA HAPA
Jarida la Forbes limetoa orodha mpya ya wanamuziki walioingiza pesa nyingi zaidi kwa miezi 12 iliyop...Read more »
21Nov2013
No comments: