» » Huyu ndiye Msanii Aliyejitangaza Kuwa Shoga Na Sasa Amebadilisha Jina Lake

Ni maarufu kama Frank Ocean kwenye muziki duniani na mara ya kwanza alivyotangaza kuwa anashiriki mapenzi ya jinsia moja alipata umaarufu mkubwa na kufanya collabo na wasanii wakubwa kama Jay Z kutoka Marekani.



Taarifa mpya kutoka kwake ni kwamba jamaa sasa amebadilisha jina lake na kuamua kuitwa Frank Ocean ambalo ni jina analotumia kwenye muziki tu. Fahamu kuwa jina lake halisi ni Christopher Edwin Breaux .


Kwa mujibu wa sheria za Marekani ni lazima Frank atangaze kubadilisha jina kwenye magazeti mara nne kwa wakati tofauti ili kukubaliwa kuanza kulitumia kama jina lake halisi. Anaweza kufanya hivyo mara moja kwa wiki kwa mfululizo wa wiki nne.


Sababu ya kufanya hivi ni kuhakikisha kuwa kama anatumia jina Frank Ocean kutapeli mtu basi ataweza kujitokeza na kufikisha kesi yake mahakamani.

Tunaomba Maoni yako Hapa :

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply