» » Tiwa Savage tayari kwa harusi Dubai

Staa wa muziki kutoka nchini Nigeria, Tiwa Savage yupo katika hatua za mwisho kabisa za maandalizi ya harusi yake rasmi na meneja na mwenzi wake Tunji ’T-Billz’ Balogun, ambapo kwa sasa amekwishatua nchini Dubai ambapo ndipo sherehe itafanyika.



Harusi ya msanii huyu itafanyika siku ya Jumamosi, tarehe 26 baada ya ile ya kimila ambayo ilifanikiwa vilivyo kuviteka vichwa vya habari mwezi Novemba mwaka jana.

Wawili hawa wanatarajia kuweka historia nyingine kubwa kwa kufanya sherehe ya kifahari, wakifuata nyayo za 2face Idibia na mkewe Anie Macaulay ambao walifunga ndoa nchini humo mwezi Mei mwaka jana.

Tunaomba Maoni yako Hapa :

«
Next
Magazetini leo Jumamosi ya Tarehe 26/4/2014
»
Previous
Video: Msichana aliyepigwa na Chidi Benz alijeruhiwa vibaya usoni na kichwani, mtazame hapa

No comments:

Leave a Reply