» » » Sad News: Misba Mwingine katika tasnia ya Bongo Movie, Mwongozaji wa filamu Adam Philip Kuambiana afariki dunia

Mwigizaji na mwongozaji wa filamu Tanzania Adam Philip Kuambiana amefariki dunia alfajiri ya kuamkia leo (May 17).

Marehemu Adam Philip Kuambiana


Kwa mujibu wa Global Publisher, Kuambiana amefariki wakati akipelekwa katika hospitali ya Mama Ngoma iliyopo Mwenge jijini Dar es salaam, baada ya kudondoka chooni akiwa location katika hoteli ya Silver Rado iliyopo Sinza kwa Remmy.

Inadaiwa kuwa kabla ya umauti kumfika marehemu Kuambiana alikuwa akilalamika kusumbuliwa na tumbo.

Tunawapa pole wana bongo movie, ndugu, jamaa na marafiki kwa kumpoteza Kuambiana.

Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema, Amen.

Tunaomba Maoni yako Hapa :

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply