» » SHTUKA MREMBO: MAMBO MUHIMU YA KUFANYA BAADA YA KUTENDWA NA UMPENDAE...!

KATIKA MAISHA YA KIMAPENZI HAKUNA KITU KINACHOUMA KAMA KUSALITIWA, TENA KUSALITIWA KUNAKOUMA ZAIDI NI PALE UNAPOBAINI MPENZI WAKO KAMPA PENZI MTU UNAYEMJUA HALAFU UKIJILINGANISHA WEWE NA HUYO ALIYEPEWA UNASHINDWA KUELEWA KILICHOMSHAWISHI MPENZI WAKO KUMPA PENZI HUYO MTU...



Lakini licha ya kwamba usaliti si kitu kizuri, watu wamekuwa wakisalitiana, tena sana tu. Inafika wakati unashindwa kuamini kama yupo mtu ambaye hajawahi kumsaliti mpenzi wake....
Niseme tu kwamba wapo wachache waliotulia ila asilimia kubwa ya walio kwenye uhusiano ni wasaliti hata tafiti zimethibitisha hilo. Kama hali yenyewe iko hivyo, cha kujiuliza ni kwamba unapobaini mpenzi wako kakusaliti ni kipi unachotakiwa kufanya? Je, ni kuamua kunywa sumu kama ambavyo wamekuwa wakifanya wengine? Sidhani kama huo ni uamuzi sahihi.

Yafuatayo baadhi ya mambo ambayo unapaswa kuyafanya baada ya kubaini kuwa mpenzi wako amekusaliti.

Kubaliana na kilichotokea
Kama keshakusaliti ni tukio ambao limeshatokea na haliwezi kufutika. Kubali kuwa umetendwa, huzunika lakini mwisho liache lipite ili uweze kujipanga upya.
Usijilaumu
Wapo ambao wakishasalitiwa hujuta kukubali kuingia kwenye uhusiano na watu waliowatenda. Utamsikia mtu akisema “najuta kumkubalia awe mpenzi wangu”. Kujilaumu kwa namna hiyo hukutakiwi kwani kutakufanya uzidi kunyong’onyea.
Jitoe
Jifanye kama vile aliyesalitiwa siyo wewe bali ni rafiki yako kisha jiulize ungemshaurije? Ushauri ambao ungempa basi uchukue kisha uufanyie kazi.
Pima ulivyoathirika

Je, kitendo cha mpenzi wako kukusaliti kimekukosesha imani juu yake? Kama ni hivyo, unadhani una sababu ya kuendelea kuwa naye au unahisi madhara aliyokupatia huwezi kumvumilia?

Tunaomba Maoni yako Hapa :

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply