Home
»
celebrity News
»
Criss Brown
»
News
»
WIZKID
» CHRIS BROWN KAMUONGELEA WIZKID WA NIGERIA KWENYE 106&PARK YA BET, VIDEO NDIO HII
Msanii Wizkid wa Nigeria ambae amewahi kuingia kwenye rekodi ya nyimbo zake kuombwa na wanafunzi kwenye show ya Club 10 Clouds FM anazidi kupata mashavu ya staa wa dunia mwimbaji Chris Brown.
Mara ya mwisho Wizkid alikula shavu baada ya Chris Brown kumuita kwenye stage na kufanya nae show kidogo wakati akiwa Ghana wiki kadhaa zilizopita lakini sasa hivi CB amempa shavu Wizkid kwenye interviw aliyofanyiwa na show kubwa ya burudani ambayo ina mashabiki mamilioni vijana kutoka sehemu mbalimbali za dunia ya 106 & Park ya Television ya BET.
Kwenye hii video hapa chini, kuanzia kwenye dakika ya nne na sekunde ya 30 wakati CB akizungumzia Album yake, aliizungumzia staili ya kucheza ya Azonto ambayo anasema alifundishwa kuicheza na staa wa muziki Wizkid kutoka Nigeria, namkariri akisema “ni staili inayotaka kufanana kama na ya Michael Jackson, utaiona kwenye video… vuta subira tu!! nimejifunza kutoka kwa Wizkid, sitaki kusema nimeianzisha mimi…. nimeitoa kwa Wizkid, ni msanii mkali wa Nigeria”
Hili linaweza kuwa zali kwa Wiz la mafanikio makubwa ya kuwa kwenye line moja na mastaa wa muziki duniani, inawezekana 2013 ukawa mwaka mwingine wa kuandika kwenye kumbukumbu za Wizkid manake ni siku chache tu zimepita toka rapper wa Maybach Music ya Rickross, Wale… kutumia page yake ya twitter kuonyesha waziwazi kwamba anamzimia Wizkid, ni msanii wake mkali wa Afrika na atasikika kwenye album yake mpya.
Wizkid na Wale ambae pia asili yake ni Nigeria.
Wizkid, Wale na Busta.
Tunaomba Maoni yako Hapa :
Category: celebrity News Criss Brown News WIZKID
Related Posts
Fid Q amzunguzia mama wa mtoto wake Fidelie
Rapper Fid Q amesema ni mapema sana kuzungumzia masuala ya ndoa na mpenzi wake kutoka Jamhuri ya Cze...Read more »
26Sep2015Kajala Ammwagia Zari Minoti!
KIMENUKA tena! Katika kile kinachoonekana kama ni kejeli kwa shosti wake wa zamani, ambaye sasa pic...Read more »
25Sep2015Picha: Tiffah ni Photocopy ya Baba yake Diamond Platnumz
Tiffah, mtoto wa Diamond Platnumz aliyezaa na mpenzi wake wa Uganda, Zari the Bosslady ni kama photo...Read more »
25Sep2015Je Umeshawahi Kujiuliza Kama Kuna Ugomvi Wowote Kati ya Lulu Michael na Wema Sepetu...? Lulu Afunguka Haya
KAMA unafikiri kuna ugonvi kati ya waigizaji maarufu nchini, Elizabeth Michael, ‘Lulu’ na Wema Sepet...Read more »
25Sep2015Dk. Cheni Afunguka Kumuoa Lulu!
Tangu wakati ule msanii maarufu wa filamu, Mahsein Awadh ‘Dk. Cheni’ aamue kupambana kumsaidia Eliza...Read more »
25Sep2015Mama wa Diamond Aongelea Kuhusu Mjukuu wake Kuwa si Mtoto wa Diamond
Weekend iliyopita mtoto wa Diamond na Zari aitwaye Tiffah alitimiza siku 40 na sura yake kuonyeshwa ...Read more »
25Sep2015
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments: