Inasemekana kuwa Albert, 28, alianguka nyumbani kwa marafiki zake na alikuwa amekunywa pombe zaidi ya mara tano ya kinachotakuwa kunywewa nchini Afrika Kusini ambapo kwenye damu yake kulipatikana 416mg za pombe kwenye kila milliliters 100.
Radcliffe ameeleza kuwa sababu ya Ngwair kupelekwa kwenye chumba cha wagonjwa mahututi ni pamoja na hypoxia (upungufu wa hewa ya oksijeni kwenye seli na tissue za mwili) na mmoja wa marafiki zake alipatikana na chumba mbili tupu za Vodka ziizokuwa kwenye gari.
Ripoti hiyo inadai kuwa Ngwair alikuwa na tatizo la kutokula chakula miezi kadhaa kabla ya kifo chake na pia kujirusha bila kupumzika hata kidogo. Sampuli zilizopatokana tumboni mwake zimeonesha mkusanyiko wa madawa ya kulevya mbalimbali yakiwemo Heroin,Cocaine ‘crack’ na bangi ya 0.08gms ilipatikana kwenye damu yake.
Kifo chake kilitokana na na mshtuko mkali wa moyo na kushindwa kupumua kulikotokana na moyo kuacha kufanya kazi na hivyo kupelekea kifo chake ndani ya sekunde chache tu.
SOMA TWEET YAKE YA MWISHO - EVERY SECOND OF EVERY MINUTE OF EVERY HOUR OF DAY I NEED GOD
No comments: