» » » Video ya Shakira na Rihanna yawaudhi waarabu, Wasema ni Video ya Kisagaji

Umeitizama video mpya aliyoifanya Rihanna na Shakira kama ujapata kuiona basi itazame hapa, au nyuma ya kamera ya uandaaji wa video hii kwa kuitazama hapa chini



Baada ya hapo tunaweza kundelea

Kutoka katika video hiyo uliyoitizama Kujizungusha kitandani na Rihanna huku wakivuta, Cigar, kumemweka Shakira kwenye maji ya moto.



Hivi karibuni Shakira aliachia video ya wimbo wake “Can’t Remember to Forget you” aliomshirikisha Rihanna iliyoleta tafrani kubwa katika nchi za Kiarabu. Shakira ameshutumiwa kwa ‘kupromote usagaji’ na Rihanna kwenye video hiyo.

“Ni video ya kisagaji,” Fadi Haddad, muongozaji wa video wa Lebanon alikiambia kituo cha runinga Al Arabiya News.

Shakira, ambaye asili yake ni Columbia, analaumiwa zaidi kutokana na babu na bibi yake kuwa na asili ya Lebanon na walihama kutoka Lebanon kwenda New York City, ambako baba yake alizaliwa.

Video hiyo iliyowekwa kwenye mtandao wa YouTube, Jan. 31, iliangaliwa kwa zaidi ya mara milioni 88 ndani ya wiki moja pekee na sasa imeshaangalia kwa zaidi ya mara milioni 100.

Tunaomba Maoni yako Hapa :

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply