» » 'Lady In Red Fashion Show' iliyodhaminiwa na Times FM kufanyika February 14,Serena Hotel

Onesho la Lady In Red Fashion Show,linalofanyika kwa mwaka mara moja safari hii litafanyika tena katika ukumbi wa Serena Hoteli jijini Dar es Salaam.Ijumaa ya tarehe 14 February mwaka huu.

Onesho hilo huonyesha mavazi ya wabunifu mbalimbali wakongwe na chipukizi lengo kuwajenga watanzania kuendelea kukubali bidhaa zao.



Akizungumza na waandishi wa habari leo ‘Asia Idarous’ ambaye ni mbunifu alisema mwaka huu kutakuwa na vitu tofauti ambavyo vitawavutia watu mbalimbali watakaohudhuria onesho hilo.

‘Mwaka huu wanamitendo wataonyesha ubunifu wa mavazi yao na kuyatambulisha kwa wageni wakiwa smart ambao ni Martin Kadinda,Rio Paul,Ally Remtullah,Mustafa Hassanali,Kiki Fashion,Rose Fashion,Francica Shirima.Kwa upande wa chipukizi ni Faustine Saimon,Jackson Ndumbala,Alabama King,Aneth Ngongi na wengineo,burudani tutakuwa na msanii Nemo & Ba Blue Band na nyinginezo.

Asia aliongezea kuwa sehemu ya mapato itakayopatikana itatumika kuendeleza mfuko wa kusaidia waathirika wa madawa ya kulevya.

Usiku wa Lady In Red Fashion Show utakuwa na kiingilio cha Shilingi elfu 30,000 kwa kila mtu,kwa VIP kiingilio Shilingi elfu 50,000/=

Tunaomba Maoni yako Hapa :

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply