Warembo wa Miss Utalii Tanzania 2013 wakiwa katika Picha ya Pamoja
Baada ya shamlashamla na mapokezi makubwa ya Miss Utalii Tanzania walipo ingia Mkoani Tanga na kupokelewa na umati mkubwa wa watu, warembo hao wapo kambini tayari kwa maandalizi ya Fainali hizo.
Fainali za Taifa Miss Utalii Tanzania zitafanyika Tarehe 19.05.2013 Mkoani Tanga ambapo warembo zaidi ya 30 watapanda Jukwaani kuwania Taji la Taifa la Miss Utalii Tanzania 2013 ndani ya Mkwakwani.
Sambamba na Fainali hizo za Miss Utalii , kutakuwa na Burudani ya Kukata na shoka ambayo itasindikizwa na Bendi kongwe ya Muziki Msondo Ngoma kutoka Dar es salaam, Mwanamuziki wa Kimataifa Che Mundugwao, Majuto Arts Group, Mdumange, vikundi vya ngoma na Sarakasi.
Fainali za Taifa zitaanza kuanzia saa 7 mchana hadi saa 12 jioni Ambapo viingilio kwa watoto itakuwa 2,000 na wakubwa 5,000 Baada ya hapo kuanzia saa 1 usiku hadi Majogoo viti Maalum itakuwa ni 20,000 na kawaida itakuwa 10,000
Mpaka sasa Kambi ya Miss Utalii Tanzania 2013 ipo jijini Tanga Mwambani Hotel na inaendelea Vizuri, Warembo zaidi ya 30 kutoka mikoa yote nchini ,wanajiandaa vizuri kwa ajili ya Fainali Hizo zitakazo fanyika wiki ijayo Tanga, Kanda Maalum ya Zanzibar na Vyuo vikuu Tanzania.
No comments: