Home
»
celebrity News
»
Mesen Selekta
»
News
» PRODUCER MESEN SELEKTA ADAIWA KUKIMBIA DENI LA ZAIDI YA LAKI 3 KWENYE HOTELI MWANZA ALIKOFIKIA
Mesen Selekta producer anaewania tuzo ya producer bora wa mwaka na producer bora chipukizi katika KTMA 2013, anadaiwa kuingia mitini na deni la zaidi ya shillingi laki 3 aliyokuwa anadaiwa kama malipo ya malazi na chakula katika hotel aliyofikia jijini Mwanza.
Kupitia segment ya U Heard ya XXL Clouds FM, jana (May 27) dada mmoja aliyefahamika kama mhudumu wa hotel hiyo alifunguka kile kilichotokea mpaka Jerry Katoto a.k.a Mesen Selekta kuondoka bila kulipa bill ya hotel hiyo aliyofikia.
“Eeh bwana eh sisi yani kama mwezi mmoja hivi tulipata mgeni huyo mgeni katika registration card jina lake halisi ameandika anaitwa Jerry Katoto na jina la kisanii anaitwa Mensan Selekta. Huyo kaka tumekaa naye kwanza kuna mtu alikuja kumfanyia booking, alivyomfanyia booking akatuambia huyu kaka ni producer na atakaa, tukasema hamna shida, upande wa malipo tutakuwa tunakuja kulia,” alifunguka dada huyo.
“Wiki ya kwanza kweli walilipa vizuri, ikafuata wiki ya pili tukauliza vipi malipo akasema ‘malipo usiwe na shida utakuja ulipwe’ tukasema haina shida, akaendelea kukaa akakaa akakaa. Sasa katika bill ilikuwa ni room aliyokuwa anakaa ni ya elfu thelathini, sasa deni likawa limekuwa kubwa tukamwambia ‘kaka samahani tunaomba ulipe’ akasema ‘hamna shida kuna mtu atakuja awalipe’ tukasema ‘sawa’ kwasababu ni mtu anayefahamika hawezi kutufanyia uhuni tukasema hamna shida.
Sasa siku moja bana kama siku mbili hivi zimepita, ye alikuwa ana movement za kuingia na kutoka ndani, siku aliyoondoka akaondoka jumla hakutupa taarifa kwamba naondoka hakutuambia kwamba labda nnavyoondoka kuna mtu atakuja kutulipa hakutoa taarifa yaani aliondoka mwizi unaona, mle ndani mpaka saizi nnavyokwambia kuna vitu vyake ambavyo ali…kuna suruali ya jeans na vitu vingine ambavyo mi sivijui labda wanatumia katika usanii unaona. Sasa sisi tunajaribu kupiga namba ambayo alikuwa ameiandika pale kwenye ile kadi sasa hivi ninavyoongea na wewe tumeshajaribu kupiga hiyo namba haipatikani.”
Msichana huyo ambaye ni mfanyakazi wa hotel hiyo ameomba Mensen Selekta alipe deni hilo vinginevyo itabidi dada huyo na mwenzake ndio wakatwe katika mishahara yao na boss wao ili kufidia deni hilo. Msichana huyo alisema deni wanalomdai Mesen inafika shillingi 392,000/=.
Msikilize hapa.
Tunaomba Maoni yako Hapa :
Category: celebrity News Mesen Selekta News
Related Posts
Fid Q amzunguzia mama wa mtoto wake Fidelie
Rapper Fid Q amesema ni mapema sana kuzungumzia masuala ya ndoa na mpenzi wake kutoka Jamhuri ya Cze...Read more »
26Sep2015Kajala Ammwagia Zari Minoti!
KIMENUKA tena! Katika kile kinachoonekana kama ni kejeli kwa shosti wake wa zamani, ambaye sasa pic...Read more »
25Sep2015Picha: Tiffah ni Photocopy ya Baba yake Diamond Platnumz
Tiffah, mtoto wa Diamond Platnumz aliyezaa na mpenzi wake wa Uganda, Zari the Bosslady ni kama photo...Read more »
25Sep2015Je Umeshawahi Kujiuliza Kama Kuna Ugomvi Wowote Kati ya Lulu Michael na Wema Sepetu...? Lulu Afunguka Haya
KAMA unafikiri kuna ugonvi kati ya waigizaji maarufu nchini, Elizabeth Michael, ‘Lulu’ na Wema Sepet...Read more »
25Sep2015Dk. Cheni Afunguka Kumuoa Lulu!
Tangu wakati ule msanii maarufu wa filamu, Mahsein Awadh ‘Dk. Cheni’ aamue kupambana kumsaidia Eliza...Read more »
25Sep2015Mama wa Diamond Aongelea Kuhusu Mjukuu wake Kuwa si Mtoto wa Diamond
Weekend iliyopita mtoto wa Diamond na Zari aitwaye Tiffah alitimiza siku 40 na sura yake kuonyeshwa ...Read more »
25Sep2015
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments: