Unknown
Tuesday, June 4, 2013
Mamia ya wakazi wa Dar es Salaam wakiwemo wasanii wa muziki na filamu nchini leo wamejitokeza kuupokea mwili wa marehemu Albert Mangwea kwenye uwanja wa ndege wa Mwl Julius Nyerere uliowasili kutoka nchini Afrika Kusini.
 |
Wasanii Dollo na KR Mulla
Bongo5 imeshuhudia umati mkubwa wa mashabiki wa Mangwea aliyefariki wiki iliyopita nchini humo uliokuwa na hamu kubwa ya kushuhudia jeneza lililokuwa na mwili wake.Baadhi ya vijana waliokuwa wakiiimba kwa sauti waliizingira gari iliyokuwa na mwili na kutaka walibebe jeneza kwa mkono na hivyo kuufanya msafara uliokuwa ukielekea kwenye hospitali ya Muhimbili usimame kwa muda bila kusogea. |
 |
Umati wa watu ukisubiri kuona gari lililobeba mwili wa Mangwea |
 |
Umati wa watu ukisubiri kuona gari lililobeba mwili wa Mangwea |
 |
Umati wa watu ukisubiri kuona gari lililobeba mwili wa Mangwea |
 |
Vijana hao ambao wengine walionekana wakilia kwa uchungu wamesikika wakiimba ‘Tumshushe, Tumbebe’.
Hali hiyo imepelekea kuzuka kwa vurugu iliyowapa wakati mgumu polisi waliosambazwa kuangalia hali ya usalama.
Wasanii mbalimbali wameonekana wakipokezana kubeba msalaba kuliongoza gari lililobeba mwili baada ya wananchi kuwataka washuke kwenye magari.
Mtangazaji wa Times FM, JABIR SALEH Ametweet: P funk ameamua kukimbia na kutembea na wana ili folen iende!!!much lov kwa p anakimbia hadi anatia huruma!”
|
 |
Umati wa watu ukisubiri kuona gari lililobeba mwili wa Mangwea |
 |
Mkoloni na Profesa Ludigo |
 |
Fid Q alikuwa mmoja ya wasanii waliojitokeza |
 |
Hafsa Kazinja na Quick Rocka wakiwa na simanzi |
 |
Chege |
 |
Abdul Kiba, Hafsa Kazinja na Sauda Mwilima |
 |
Izzo B akiwe mwenye majonzi makubwa |
 |
Mrisho Mpoto |
 |
Mwili wa Mangwea ukiwa umebebwa |
 |
Dr Cheni |
No comments: