Msanii Curtis Jackson maarufu kama 50 cent wa crew ya G unit hawezi kusahau siku kadhaa zilizopita baada ya kuandamwa na mambo mengi mabaya na bado yameendelea kumkuta. Wiki iliyopita ilisemekana kwamba 50 cent amekamatwa na polisi kwa kosa la kumshambulia mwanamke ambaye amemzalia mtoto wa pili japokuwa 50 cent hakuwahi kusema kwamba ana mtoto wa pili. Lakini 50 cent alijibu kupitia instagram kwa kutumia neno “am not in jail am in” na kumalizia eneo alipo kwa mfano am not in jail am in my living room kama ulivyosoma kwenye stori iliyopita ya 50 cent hapahapa.
Baada ya kashfa hiyo ya kumshambulia baby mama wake, 50 cent alitoswa kufanya show ya MLB. Mambo yanazidi kumuendea mrama 50 cent, hivi sasa kwenye internet habari kubwa ni kuhusu msanii huyu kumtumia sms zenye lugha chafu mtoto wake wa kiume ambaye ana miaka 16 tu. Hivi sasa Marquise ambaye ndiyo mtoto wa 50 cent anaishi na mama yake na wakati anachat na baba yake ambaye alimtupia maneno machafu sana alikuwa nyumbani kwa mama yake.
Baada ya hizi screen shot za maneno ambayo msanii huyu alimtumia mwanaye na baadaye zikavuja kwenye internet, 50 cent aliingia kwenye ukurasa wake wa twitter na kuandika kwamba aliyekuwa anajibu hizo sms ni mama yake Marquise ndiyo alikuwa anajibu na siyo mtoto huyo. Hakuishia hapo lakini aliendelea na kusema kwamba baada ya maongezi yale, ameamua kwamba Marquise sio mtoto wake tena na anamtoa kwenye list ya watu atakao wapa urithi wake. 50 cent akazidi kungezea kwamba anahitaji kufanya DNA test kuhakikisha kama huyu mtoto ni mwanaye kweli au la, kwasababu anawasiwasi kama mama yake Marquise alim-cheat kipindi hicho wanapata huyu mtoto.
Baadhi ya mitandao imehoji kuhusu haya maneno machafu ambayo 50 cent ameyatuma kwa mtoto mdogo wa miaka 16 tu, pia kwa nini amemtoa kwenye list ya urithi wake kisa ameonyesha kutokuwa na heshima kwa baba yake wakati baadaye 50 cent ame-tweet kwamba aliyekuwa anajibu ni mama yake na sio Marquise. So hakuna sababu ya kumfuta Marquise kwenye list ya watu watakaopata urithi kwa kumkosea heshima baba yake ikiwa aliyekuwa anajibu zile sms ni mama yake.
Hizi ndiyo screen shoots za sms alizotuma 50 cent kwenda kwa mtoto wake ambazo hadi sasa 50 cent hajakataa kama sio sms zake bali alichokisema ni kwamba aliyekuwa anajibu hizi sms ni mama yake Marquise akitumia simu ya Marquise
No comments: