Home
»
ali Kiba
»
celebrity News
»
News
» Hivi Unajua Kuwa: Nyimbo za Ali Kiba zinasikilizwa zaidi Muscat ‘huenda’ kuliko msanii mwingine wa Bongo Flava
Anaweza asiwe na hit redioni kwa sasa lakini Ali Kiba ndiye msanii wa Tanzania ambaye nyimbo zake zinasikilizwa zaidi mjini Muscat, Oman, kwa mujibu wa Mtanzania aishiye huko.
Bongo61 ilikuwa ikichat leo na Mtanzania huyo, Rayya Al Habsi. Ameiambia kuwa muziki wa Bongo Flava unasikilizwa mno nchini humo hata na watu wasiojua kabisa Kiswahili.
“Bongo fleva muscat inapendwa sana, ninafahamu wengi ambao hawafahamu Kiswahili lakini kwenye magari yao wanapiga nyimbo za Ali Kiba, amesema Rayya.
Mbali na Ali Kiba, amesema wasanii wengine wa Bongo Flava wanaopendwa ni pamoja na Diamond, Ommy Dimpoz na Dully Sykes wengine wanapenda zaidi mduara kama nyimbo za Kilimanjaro Band, AT na Off Side Trick.
“Ukija kwenye band Twanga Pepeta imekuja huku mara nyingi na show zao zilikuwa Muscat Festival.”
Ameongeza kuwa wasanii wa Tanzania wanaofanya hip hop hawana umaarufu kama walivyo waimbaji nchini humo.
“Sina hakika kuhusu hip hop japo nakumbuka wakati wa kina GK na AY watu walikuwa wanasikiliza nyimbo zao. Hapa muscat wengi wanapenda nyimbo rahisi kufaham na lugha imetumika ni ya kawaida. Sasa mziki wa kuimba ni rahisi kuusikiliza,” amesema.
Mwezi ujao TID anatarajiwa kwenda kufanya show mjini Muscat.
Tunaomba Maoni yako Hapa :
Category: ali Kiba celebrity News News
Related Posts
Music: Ali kiba ft Abdu Kiba - Pita Mbele
Sikiliza hapa wimbo mpya kutoka kwa kiba Square unaoitwa Pita Mbele, sikiliza na kuudownload hapa&nb...Read more »
17Jun2014Picha: Haya ndiyo Majibu ya ukimya wa Alikiba utayapata soon, aanza rehearsal ya video mpya
Alikiba amekuwa akiulizwa maswali mengi kuhusu lini anatoa kazi mpya sababu amekuwa kimya kwa muda m...Read more »
20May2014Siri nzito inayomfanya Ali Kiba kuzidi kupendwa zadi na Bongo
Wasanii wengi wa fani mbali mbali kuanzia filamu hadi bongo fleva, wamekuwa wakipoteza mashabiki wao...Read more »
26Apr2014Makala: Kwanini Ali Kiba hawezi kuja Kushuka kimuziki...
Leo katika makala yetu tunamuongelea ali kiba au a.k.a Kiba 4 Real Mwanamuziki wa Bongoflavour na al...Read more »
16Jan2014Huyu Ndiye Mpenzi wa Ali kiba ..ni Mrembo na Anavutia kiukweli
Ally Kiba anaweza kuwa hasikiki sana kwenye redio miaka ya hivi karibuni na humsikii akilalamika. Hu...Read more »
13Jan2014Picha: Mfahamu mtoto wa kiume wa Ali Kiba
Ali Kiba ni miongoni mwa wasanii ambao tayari wanaitwa baba, kuna uwezekano hujawahi kumuona mtoto w...Read more »
05Jan2014
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments: