Msanii wa Hip Hop na mshindi wa tuzo 3 za KTMA 2013, Kala Jeremiah amefunguka kwa kuandika waraka mrefu kuelezea jinsi anavyomkubali waziri mkuu wa zamani Edward Lowassa kwamba anafaa kuiongoza nchini.
Usome waraka wake huo wote;
Mimi Kala Jeremiah nilikuwa msanii wa kwanza Tanzania kumsema mheshimiwa Edward Lowassa kupitia wimbo wangu uitwao wimbo wa taifa baada ya mheshimiwa kukumbwa na kashfa ya ufisadi wa Richmond.Kwa kipindi kile kila mmoja wetu alihamaki sana na kuona kweli mzee wa watu ni fisadi.Kwenye wimbo huo kuna mistari nilisema, ‘mi siyo mwana siasa sisubiri tume ichunguze nistaafu ka Lowassa.
Kwa kuwa mimi ni mzuri sana kwenye kufanya uchunguzi binafsi nilitumia muda mwingi sana kulichunguza swala hili la kashfa hii na baadae niligundua kuwa ni swala la kisias, na yalikuwa ni mapito ambayo mwanadamu yoyote hupewa muda wa kupitia magumu ili kupimwa imani yake kwa Mungu.
Baada ya kugundua hayo mwaka jana nilitengeneza wimbo unaoitwa ‘Azimio la Arusha’ ambao upo kwenye album yangu ya Pasaka ambayo iko sokoni tokea mwaka jana. Katika wimbo huo wa Azimio la Arusha niliandika mistari ifuatayo, walipiga dili waka msakizia Lowassa ili kuficha siri kali.
Niliandika mstari huu baada ya kufanya uchunguzi na kujiridhisha kuwa mheshimiwa ni kiongozi bora sana na hasa kwa uamuzi wake wa kujiuzulu bila shinikizo kubwa na wakati kwa nafasi aliyokuwa nayo ya uwaziri mkuu alikuwa na uwezo wa kugoma kujiuzulu na hasa kwa kuwa hakuwa fisadi kama ilivyosemwa.
Mwezi wa tatu mwishoni mwaka huu nilitoa wimbo unaokwenda kwa jina la Karibu Dar ambako nilisema ‘Dar es Salam ingekuwa nchi rais angekuwa Lowassa huku watu washashtukia kuna mchezo kwenye siasa’, hapa nilikuwa namaanisha kuwa watu wengi wanaoishi Dar wanawahi kujua mambo ya wanasiasa kwa kuwa wanasiasa wanaishi huku lakini pia watafiti wengi wa mambo ya kisiasa wanaishi huku kwa hiyo ni rahisi zaidi kuujua ukweli mapema.
Naamini kuondoka kwa Lowassa kwenye uwaziri mkuu kumezorotesha maendeleo ya taifa kwa kiasi fulani.
Ndugu zangu watanzania ni wazi kuwa Lowassa ni jembe tena jembe la kazi kumbukeni bila Lowassa kusingekuwa na shule za kata Tanzania,na angeendelea kuwepo madarakani alikuwa na mpango wa kuanza mchakato wa zahanati za kata, ikumbukwe pia Lowassa ndiye aliyesimamia ujenzi wa chuo cha udom tena kwa pesa za kitanzania bila kuombaomba vimikopo.
Mradi wa maji kutoka Mwanza kwenda Shinyanga ni kazi ya Lowassa, zipo kazi nyingi ambazo nikizitaja zote naweza kujaza ukurasa.Nachojaribu kusema hapa ni kwa kuwa mimi ni msanii na ni kioo cha jamii ningeomba wewe mwanajamii chukua hatua ya kufanya uchunguzi binafsi kuhusu Lowassa, bila kufuata mkumbo wa kisiasa naamini utakubaliana na mimi kuwa Lowassa ni jembe.
Mimi huwa napenda kusoma vitabu vya wanaharakati na kuna kitabu kimoja nilikipitia cha mwanaharakati kutoka Italy aitwae Niccolo Machiavelli ambaye alizaliwa mwaka 1469 na kufariki 1527. Katika enzi za uhai wake aliwahi kuandika vitabu kadhaa lakini kati ya vitabu hivyo kitabu kiitwacho ‘The Prince’ ndicho kilimpa heshima kubwa sana kwa kuwa aliikosoa serikali ya kifalme ya kipindi hicho kitu ambacho hakikuwa rahisi kwa mtu kufanya hasa ikikumbukwa kuwa enzi za ufalme zilikuwa enzi za ubabe.
Katika maneno kutoka kwenye kitabu hicho ambayo ninge penda kukushirikisha wewe ndugu yangu Mtanzania ni maneno yafuatayo,machiavelli aliandika hivi: ‘Kuna kipindi ambacho mataifa yanapita katika vipindi vigumu, na kwa kipindi hicho kigumu mataifa hayo yatahitaji sana kupata kiongozi mwenye kuweza kuchukua maamuzi magumu,na ambaye hatakuwa chini ya sauti ya mtu mwingine, na ambaye ataweza kuyatekeleza maamuzi magumu kwa haraka hata kama ni kwa kuwaumiza wachache ili wengi wawe huru.
Atakayekuwa tayari kutekeleza jambo baya ili likapita na kusahaulika na atakayetekeleza mambo mazuri kwa muda mrefu na yakaendelea kukumbukwa. Kiongozi huyo atatakiwa kuchagua kuogopwa ama kupendwa lakini ni bora akachagua kuogopwa lakini akitenda haki kwa wananchi husika.’
Hayo ni baadhi ya maneno aliyoandika na Machiavelli kwenye The Prince, kitabu ambacho kilimpelekea kuitwa na mfalme na kupewa nafasi ya juu ya uongozi katika serikali hiyo ya kifalme.
Kwa maoni yangu nadhani taifa letu limepitia vipindi vigumu kadhaa na kwa maneno ya Bwana Machiavelli nadhani kiongozi anayefaa ambaye anaweza akachukua maamuzi magumu na ambaye hawezi kuwa chini ya sauti ya mtu mwingine ni mheshimiwa Edward Ngoyai Lowassa.
Kuna watu wanasema nimenunuliwa sijui nimepewa pesa. Mimi kama mkristo niliyebatizwa kwa maji mengi naapa sijawahi kumjua Lowassa kuonana naye wala kuwasiliana naye zaidi ya kumuona kwenye TV.
Ila nimejisikia kuongea haya kwa sababu watu wengi tunafuata yanayosemwa na wanasiasa hatuangalii nani aaaweza akafanya nini kwenye taifa letu.Mimi nina mashabiki na mashabiki wangu ndiyo maboss wangu nitafurahi sana kama maboss wangu watapata maisha bora na kwa kupitia maisha bora ya mashabiki zangu na mimi nitakuwa na maisha bora.
Amini hakuna mwana siasa anaweza kumnunua Kala Jeremiah kwa senti ingekuwa hivyo ningeshanunulika miaka hiyooo. Narudia tena Lowassa ni jembe.
Wanaosema nimehongwa mwaka jana wakati naenda studio kurecord wimbo wa Azimio la Arusha ambao ndo ulikuwa wimbo wangu wa kwanza kumtetea Lowassa, nilienda studio kwa daladala. Mwaka huu mwanzoni wakati naenda studio kurecord ‘Karibu Dar’ niliendaaa studio kwa daladala.
Mpaka sasa napost post hii mimi ni msanii bora wa hip hop lakini sina gari, wanaonifahamu kwa karibu wanalijua hilo. Je kama fisadi kaninunua kanilipa elfu kumi au?
Najua mtakuja kuelewa baadae nafanya hivi kwa ajili ya kulilia wananchi maskini wenye ndoto za kuishi maisha bora.
Halafu Lowasda sio mtu wa kwanza mimi kumsifia. Nilishaawahi kuwasifia Dr Slaa, Zitto Kabwe,Mwakiembe, basi ingekuwa ninakusanya hela basi ningekuwaa milionea mkubwa sana kwa sasa.
No comments: