Mama mzazi wa aliyekuwa muigizaji wa filamu, mchekeshaji na muimbaji, marehemu Hussein Ramadhani aka Sharo Milionea ameendelea kuingia hofu juu ya kupotea kwa baadhi ya mali alizoacha mwanae.
Akiongea na Bongo61, aliyekuwa rafiki yake kipenzi, Kitale amesema mama yake Sharo ameingiwa na hofu baada ya kuona kimya kutokana na ahadi alizopewa baada ya matanga na kwamba kuna mali ambazo alitakiwa kukabidhiwa.
“Mali ambazo aliahidiwa mama Sharo ni gari aina ya Oppa ambayo ina thamani ya milioni 16 na marehemu Sharo aliazima gari la aina ya Toyota Harrier ambalo alipatanalo ajali lililokuwa na thamani ya milioni 25 ila jamaa mwenye Toyota Harrier ile siku ya matanga aliomba akabidhiwe Oppa aitumie Halafu baadaye atamkabidhi mama Sharo ila kwa bahati mbaya mpaka leo mama Sharo hajakabidhiwa gari, ndiyo maana yule mama anakuwa na wasiwasi, sasa baadhi ya watu wanadhani mimi nashikilia hizo mali wakati ndivyo sivyo,” amesema Kitale.
“Sharo alikuwa anamiliki gari aina ya Oppa na Bajaj, mimi kuna filamu ya mwisho niliyofanya na marehemu Sharo na kwa makubaliano yetu tukija kuuza tuweze kugawana mapato kwahiyo watanzania watambue hivyo.”
No comments: