Kampuni moja ya Uingereza imeendesha shindano la kutafuta mnyama anayevutia zaidi katika picha ‘The most photogenic animal’ wa Uingereza, na huyu ndiye aliyeibuka mshindi.
Mbwa huyo aitwaye Rylo aliwabwaga washindani wake wengine 25 na kukamata nafasi ya kwanza na kuvishwa taji hilo.
Katika mchuano huo, washiriki wote (wanyama) walipozi na kupigwa picha kama njia ya kutafuta mshindi, na pozi za kununa za Rylo ndio zilizompa ushindi sababu zimefanya kuwepo na upekee katika picha zake.
Wamiliki wa mbwa huyo Craig Howlett-Wright na David Birks wamesema wamefurahi sana kwa kiumbe wao kushinda na hawaamini amewamwaga wapinzani wake 25, pia wamezawadiwa kapu lililojaa zawadi kwa kazi ngumu waliyoifanya kwa mbwa wao, hahahaha (funny right?)
SOURCE: DAILY MAIL
No comments: