Polisi walikuwepo ili kulinda usalama kwenye eneo la tukio
Mmoja wa majeruhi akipandishwa kwenye gari
Ajali mbaya nyingine imetokea jana usiku katika mlima kwa Kitonga wilaya ya Kilolo mkoani Iringa katika barabara kuu ya Dar es Salaam -Iringa .
Katika ajali hiyo watu wawili wamekufa papo hapo huku wa wawili wakijeruhiwa vibaya baada ya malori mawili kugongana uso kwa uso .
Ajali hiyo imetokea mida ya saa 12.50 jioni ya jana ikiwa ni dakika takribani 30 baada ya ajali ya basi la JM kupinduka eneo la Mazombe wilaya ya Kilolo.
Chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa lori la IT lililokuwa likisafirishwa kwenda nchi za kusini mwa Tanzania aliyekuwa akitaka kulipita gari la mbele mlimani na katika kona kali .
Hata hivyo dereva wa lori hilo IT aliyetambuliwa kwa jina la Gody amevunjika mguu wake ambao umetoka na dereva na utingo la fuso wamekupa papo hapo huku mwanamke aliyekuwa katika lori IT akisalimika .

Chanzo:Sanga festo
No comments: