Siku mbili zimepita tangu, mfalme na malkia wa drama Bongo, Diamond Platnumz na Wema Sepetu wakinukishe tena. Hakuna kipya zaidi ya nini kimeendelea baada ya kusambaa kwa picha za Diamond na Wema wakila raha Hong Kong.
Lakini, la uhakika ni kuwa, kwa sasa kuna mpasuko mkubwa katika kambi zao. Story za mtaani ambazo binafsi Bongo5 haijaweza kuzithibitisha ni kuwa, kuna ugomvi mkubwa kati ya Wema Sepetu na mwanaume anayedaiwa kuwa ni mpenzi wake wa sasa.
Labla kukupdate tu ni kuwa baada ya Wema Sepetu kuachana na Diamond, ama tuseme baada ya wapenzi hao kupumzika kuwa pamoja kwa muda, Wema Sepetu aliendelea na maisha yake na ofcourse alipata mwanaume mwingine ambaye hajawahi kujulikana wazi ni nani. Diamond pia aliendelea na maisha yake na kuanzisha uhusiano na Penny.
Lakini, mitaa inasema kuwa wawili hao walikuwa wakiendelea kumegana kisela. Ndio maana yale maongezi yao ya simu yalivuja, ikiwa ni ishara kuwa walikuwa bado na mawasiliano mazuri. So mitaa inasema, jamaa anayesemekana kutoka na Wema kwa sasa, amemind vibaya mno, na tangu kusambaa kwa picha hizo, hakuna amani tena.
Picha hizo zilimaanisha kuwa, Penny hakuwa muathirika pekee wa picha hizo, bali pia Wema ameuvunja moyo wa mwanaume anayedaiwa kumpenda kwa dhati. Mashemeji na mawifi nao wametengeneza kambi zao, Team Penny vs Team Wema.
Nini kinaendelea sasa?
So far, hakuna kipya cha kuthibitisha, ukizingatia kuwa hakuna hata mmoja kati yao ameshaongea japo itafika siku wataongea, siku ambayo watakuwa wamepata maelezo mazuri ya kuushawishi umma kuhusu kile Diamond anakiita filamu.
Lakini kwa kutazama picha za Instagram za watatu hao, Diamond, Wema na Penny, maisha yanaendelea na wote wanaonekana wapo vizuri, kama hakuna kilichotokea japo kile ukionacho kwenye mitandao ya kijamii, ni tofauti kabisa na hali halisi.
Diamond
Kwa siku hizi mbili, Diamond amekuwa akipost picha za bling bling tu, akifanya shopping za nguo na vitu vingine vya gharama.
Wema
Kwa mujibu wa kile alichokiandika kwenye moja ya picha zake za leo, Wema amefiwa na babu yake.
“We loved you, we love you and will always love you…. it hurts to lose such a character, you were a man of god.. always taught us how to abide by da rules of Allah… Today u are gone and it kills me inside to know dat I will nat see you again but there is a relief in me dat you are now in a better place… with da angels… because even if we couldnt see dem, but they were always around you…. I love you my babu… il aleays remember you wit your saying “babu kababuka” … oh my God it hurts…. You are always going to live in our hearts…. Rest In Eternal Peace Mzee Athmann Sumbe… im sure you are now smiling and sooo happy werever you are… A man wit a pure soul ryt here,” ameandika.
Picha nyingine inamuonesha akiwa na simu ile ile aliyopiga nayo Diamond kwenye picha zake. Inaonekana wana simu ya aina moja, Samsung nyeusi.
Penny
Penny na Wakazi, jana usiku DTV
Penny anaonekana yuko poa, walau kwa picha iliyowekwa na rapper Wakazi kwenye Instagram ikimuonesha akicheza muziki kwa furaha, like nothing happened.
“I had a blast last night on the XTreme Show on DTV with baby girl @vjpenny04 & DJ Pack. Thank you so much for those who watched the show and I hope you enjoyed as much as we did.,” aliandika Wakazi kwenye picha hiyo. Ama hiki ndio kama kile John Legend alikiimba kwenye Dancing The Pain Away.
“Ohh, Everybody’s going to the floor
Maybe I don’t want to dance anymore
Don’t want to dance anymore
How can you dance the pain away
How can you dance the pain away
Oh dance the pain away
I can’t dance the pain away
How can you dance the pain away
How can you dance the pain away
Oh dance the pain away
I can’t dance the pain away”
News via:Bongo5
No comments: