» »Unlabelled » Peter Okoye wa P-Square kufunga ndoa na mchumba wake Lola (November)



Kama pesa wanayo, watoto wanao, na pete tayari sasa na kifuatacho ‘Squareville’ ni….ndoa. Kama unakumbuka miezi miwili iliyopita Peter Okoye wa kundi la P-Square kutoka Nigeria alimuuliza babymama wake Lola Omatayo swali muhimu katika uhusiano wa kimapenzi la ‘will you marry me?’, na of-course alipewa jibu adimu la ‘YES’ kutoka kwa Lola.

Wapenzi hao wa muda mrefu Peter na Lola wanatarajia kufunga ndoa ya kimila tarehe 17 November huko Lagos Nigeria, na baadaye wanampango wa kufunga ya kanisani mwakani 2014. Kwa mujibu wa Nigeria films.

Wakati wa kumvisha pete ya uchumba mwanzoni mwa mwezi wa nane mwaka huu Peter alimzawadia baby wake gari aina ya Range Rover SUV. Peter na Lola wamefanikiwa kupata watoto wawili ambao watakuwa mashuhuda wakubwa wa muungano wao rasmi wa kuwa mwili mmoja.

Tunaomba Maoni yako Hapa :

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply