Mabosi wa Twitter wameanzisha tena vita vya maneno dhidi ya Facebook kwa kudai kuwa wanachofanya wao ni kutawala, kuharibu na kuvunja vitu.
Mkuu wa kitengo cha habari cha Twitter, Chloe Sladden, anadai kuwa Twitter ilikuwa mtandao wa kijamii mbadala na muhimu kwasababu ulikuwa bora zaidi katika kutengeneza kile alichokiita ‘shared experience’.
Mkuu wa kitengo cha habari cha Twitter, Chloe Sladden
Aliongeza pia kuwa Twitter ilishinda vita ya kile alichokiita hitaji la msingi la kuwasiliana’ ijapokuwa Facebook ina watumiaji wengi zaidi. Twitter na Facebook wamekuwa na uhasama tangu mwaka 2008 pale Facebook ilipotaka kuinunua Twitter kwa $500m lakini ikakataa.
Uhusiano uliendelea kuharibu zaidi mwezi April pindi Twitter ilipojaribu kuinunua Instagram lakini Facebook ikainunua kwa kutoa cha juu zaidi, na kuinunua Instagram kwa $1bn.
Baada ya hapo Instagram iliondoa kitu kilichowezesha picha za mtandao huo kuonekana moja kwa moja kwenye Twitter.
Kisha, mapema mwaka huu, Facebook ilianza kutumia hashtags na kuonekana kama tusi la wazi kwa Twitter, waanzilishi wa vitu hivyo
No comments: