» » » » Ukimtaka King Majuto katika Filamu yako au Kumshirikisha ni Tsh Milioni 10



Unamtaka King Majuto kwenye filamu yako? Una shilingi milioni 10? Basi tunaweza kuongea. Kwa mujibu wa msemaji wa muigizaji na mchekeshaji huyo ambaye pia ni mwanae, Hamza Majuto, gharama ya kufanya filamu na Mzee majuto imepanda mara tatu hadi kufikia shilingi milioni 10 kwa sasa.


Hamza alisema walikuwa wanafanya filamu kwa milioni 3 mpAka 4 ila kwa sasa imepanda kutokana na maHitaji ya Mzee Majuto Kuongezeka kila siku.

“Ile bei ambayo tulikuwa tunafanya imepanda mara 3 au 4 kwa sasa atakaye muhitaji ni milioni 8 mpaka 10 kutokana soko la filamu kwa upande wa uchekeshaji, hata hivyo filamu zake zimekuwa zikifanya vizuri sokoni,” alisema.

Miezi 8 iliyopita katika kipindi cha Mkasi, Mzee Majuto alisema anahitaji kupandisha bei mpaka kufikia milioni 3 mpaka 5 kutokana filamu zake kuwa nyingi mtaani akiwa na imani kuwa zinaweza zikampunguzia mashabiki kutokana na kuonekana mara nyingi katika filamu.

Tunaomba Maoni yako Hapa :

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply