Muigizaji wa filamu na mchekeshaji nchini, Amri Athuman aka King Majuto ametangaza nia ya kugombea Ubunge wa Tanga Mjini mwaka 2015 ambapo amesema anataka kuinua uchumi wa Tanga pamoja na kutetea haki za wananchi na rasilimali za mji huo.
Akizungumza na Bongo5 leo kwa njia ya simu akiwa nyumbani kwake Tanga, Majuto amethibisha kugombea ubunge mwaka 2015 kwa tiketi cha CCM.
“Nitarudisha heshima ya Tanga ya zamani ambayo ilikuwa inasifika sehemu mbalimbali kutokana rasilimali zilizopo ambazo kwa sasa zimeshindwa kusimamiwa na kuwanufaisha watu wa Tanga,” alisema Majuto.
“Nimejipanga kwa upinzani nitaokutana nao kwasababu mimi ni mzee wa makamu naelewa mambo yatakuwaje ndio maana nimejipanga kufanya hivyo wala sijakurupuka.”
Katika hatua nyingine, Majuto ambaye ni baba wa watoto nane, amesema bado anaigiza na kwa sasa ana kikundi cha vijana nyumbani kwake ambacho anakifundisha sanaa ya uigizaji ili kutoa nafasi ya ajira kwa vijana wengine.
No comments: