» » D-KNOB AFUNGUKA NA KUTOA SABABU INAYOFANYA WASANII WENGI WAKONGWE WASHINDWE KUHIT TENA SASA


D- KNOB amesema wasanii wengi wakongwe wanashindwa kufanya vyema katika gemu la muziki kutokana na kushindwa kuendana na mabadiliko ya muziki wa sasa.



Akipiga stori na ‘Chumba Cha Sindano’ kupitia kipindi cha’ Kali za Bomba’ cha Bomba FM 104.0, Mbeya D- KNOB ameeleza kuwa baada ya kushtukia ugumu wa gemu aliamua kwenda chuo kujiongoza kielimu.

“Kwa mfano mimi sijarekodi nyimbo kitambo kwa sababu baadaye niliamua kurudi chuo na nimejiajiri mwenyewe kwa kutumia elimu ambayo ninayo na inanigea hela ndio maana watu wakiniuliza nitarudi lini katika gemu, nawaambia ‘daaah mwakani nitatoa ngoma mbili tatu’. Kwa hiyo sitoi nyimbo ili nipige hela natoa nyimbo kwa sababu na love na gemu, system ya muziki bado haijakaa vizuri,” alisema.

“Kwa hiyo utakuta watu wengi wanafanya gemu halafu ikifika age fulani wakishafika utashangaa automatic wanaacha kufanya gemu wanaacha kufanya muziki wanafanya maisha mengine ambayo wanakuwa na uhakika nayo na hela. Unajua wasanii wengi ambao wewe huwasikii si kwa sababu ya gemu imewatupa wameamua kufanya maisha mengine, wengi wanafanya hivyo kwa sababu gemu haiwatoi watu na kuwapeleka kule ambako wanatamani kwenda tofauti na enzi zile. Afadhali sasa hivi kidogo watu wanapiga show wanapasa hela, Tanzania sasa hivi mtu bado hawezi kuuza single tofauti na Kenya mtu akitoa single inampa pesa nyingi au tofauti na nchi nyingine mtu akitoa single kwenye maringtone tu anaweza kuishi kwa tutegemea ringtone, biashara ya ringtone. Sasa hivi bado ni tete ni biashara ya magumashi kwa mfano bongo mtu anayetengeneza pesa ni Diamond tu.”

D-Knob alisema kwa sasa anafanya kazi ya masuala ya usimamizi wa mipango ya miradi mbalimbali.

“Mimi sasa hivi bwana nilikuwa naiweka vizuri kampuni yangu ya Mitaani Most Wanted inajihusisha zaidi na burudani kidogo na hasahasa uandaaji wa Miradi kwa sababu nimesomea hasa masuala ya miradi(Project Plan Management), na watu ambao nafanya nao kazi sasa hivi ni Marco Chali Foundation kwa kupitia Zantel, nafanya kazi na akina Lamar.
Kwa kifupi Chama cha Sound Engineering Tanzania sasa hizo kazi wanaweza kuingia katika tovuti ya ww.mitaanimostwanted.co.tz wataona kitu gani nafanya sasa hivi nimeshaanza kuona matunda yake. Nilikuwa nataka niwe na maisha nje ya music niwe na uhakika kwanza na maisha ndio nirudi katika gemu.”

Via: Greyson Chris Bee (Bomba FM)





Tunaomba Maoni yako Hapa :

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply