Leo wakati nakuja hapa nilipo muda huu nilikuwa nimeongozana na wadada kama wa-4 hivi inaonekana wanaishi jirani na wanakofanyia kazi au kuishi ni kumoja
Wadada hawa walikua na story iliyovuta masikio yangu na kunifanya nipunguze spidi ili niendelee kuwasikiliza kwa kuwa tulipokuwa pana ka umbali kidogo hadi ufikie kituo cha usafiri wetu wa umma[Hiace/daladala/vifordi]
Wadada hawa walikuwa wanamzungumzia mwenzao ambae inaonekana siku za karibuni ataolewa
Tatizo halikuwa kuolewa bali anaemuoa
Inasemekana kuwa huyo mume mtarajiwa wa rafiki wa hao akina dada hajawahi kufanya ngono,yaani ni bikra wa kiume
Wadada wale walikuwa wanamlaumu mwenzao kwa kutokusikiliza maelekezo yao kwa kukataa kuolewa na huyo jamaa kwakuwa ni "mshamba" yaani hayajui mapenzi kitendo kitakachomfanya rafiki yao aanze kutembeza shule kwa huyo mume namna ya kugegeda kitendo ambacho wale wadada hawakukubaliana nacho
Walionekana kukerwa sana na walikuwa wanasema wao hawawezi kuja kuolewa au kuwa na mahusiano na mwanaume wa aina hiyo
Story hiyo ikanikumbusha miezi kadhaa iliyopita nilikuwa nazungumza na jamaa zangu kuhusiana na suala hili ambapo kuna jamaa alikuja kutulalamikia kuhusiana na mkewe kutokujua mapenzi kwa sababu alimkuta bikra
Jamaa yetu yule alionekana kukereka sana na alifikia kusema kama angejua asingemuoa
Kati ya vijana tuliokuwa pale watatu walikubaliana na yule jamaa
Nilishangaa!
Nilidhani kuwa kama ukimkuta mwanamke sio used basi unafurahi kumbe sio
Sasa nikiunganisha na hili tukio la leo naona hili jambo kama linakua flani hivi,yaani huenda hili suala hapo siku za nyuma lilikuwepo lakini inaonekana linachukua kasi mbaya
Nimeamua kulileta hapa ili nijue Wanaume wa hapa wanalichukuliaje suala hili
Pia wanawake nao wanalichukuliaje hili
Yaani kama kuna watu wawili ambao unatakiwa uchague kati ya huyo mmoja awe mwenzi wako na mmoja ni used na mwingine sio,ungependa yupi awe mwenzi wako na kwanini?
Watu wa siku hizi inaonekana hawapendi masuala ya kuanza kufundishana,wanataka watu ambao ni waalimu tayari
Inaonekana sisi mabikra tutaipata mwaka huu....lol!
Naomba mchango wako tafadhali!
Via Udaku
No comments: