Nisher amemdiss Adam Juma? Hilo ndio swali kila mmoja ameendelea kujiuliza bila kupata jibu. Kwa watangazaji na waandishi wa habari kama mimi tulikuwa wa kwanza kupiga simu kumuuliza Nisher kama kweli alichokiandika amemaanisha ama ni lugha tu ziligogangana na kila mtu kuibuka na maana yake.. Hata hivyo hakutaka kuliongea hilo mapema na hivyo wengi kushindwa kumpata.
Aliandika nini?
Ni maneno yaliyoandikwa kwenye karatasi na kupigwa picha yasemayo: I’m not next level, I’m a new game’. ‘Next Level’ ni jina la kampuni ya Adam Juma. Hapo ndipo utata ukaanza. Sentensi hiyo ni tata, ni metaphor. Ni kweli ameampa dongo Adam?
Nishukuru kuwa Nisher ni mtu ninayemfahamu hata kabla jina lake halijavuma kama ilivyo sasa. Infact mimi na Nisher tumefahamiana kipindi ambacho hajafanya hata video moja. Nilikuwa namfahamu kama producer wa muziki na muimbaji wa rnb. Hivyo, uhusiano huo wa siku nyingi na mimi ulimfanya anipige simu (baada ya kupiga na kukuta imeweka busy kutokana na watu wengi kumpigia kutaka ufafanuzi wa hicho alichokiandika).
Nisher alisisitiza kuwa kamwe ujumbe huo haukuwa na lengo la kumponda Adam na kwamba watu wamemwelewa vibaya. Alisisitiza kuwa kama kosa lake ni kutumia neno ‘Nexl Level’ ambalo ni jina la kampuni ya Adam, basi hata rapper Game au supermarket ya Game ingemuelewa vibaya pia.
Kwenye Instagram pia Nisher alifafanua:
“Oh so u own the Phrase “NEXT LEVEL” now?? Mmmm weird didn’t get that memo… Cuz last time I checked it’s just an English Terminology USED WORLD WIDE… besides nobody mentioned your name, it’s not a direct message. . . so chill Tha’ €### down! Umepanic brother. . . Mbona Rapper “THE GAME” HAJANITAFUTA?
Bahati mbaya ni kuwa Adam mwenyewe hajaupenda ujumbe huo na amemind…
“Afanye kazi yake asitafute ustaa kwa chatu aliyelala. Ajitahidi wasanii wasiende Ogopa basi. Changamoto my ass. Ukimya ni upuuzi but ni busara, sijapenda hii msg, but anyway I got something for you,” aliandika Adam kwenye Instagram. “On that note atafute mchiriku na mduara mmoja tuone creativity. In the end if you good I will respect you.”
Hakuna shaka sasa hivi Nisher na Adam haziivi tena.
Historia yao ikoje?
Niliwahi kukutana na Adam Juma miezi kadhaa iliyopita na kumuuliza machache kuhusiana na video za Nisher. Na ukweli wa kumuuliza swali hilo ulitokana na mabishano chanya niliyofanya na Nisher kuhusiana na video ya Ben Pol, Jikubali. Tatizo langu na Nisher enzi hizo lilikuwa ni rangi aliyokuwa akiitumia, hivyo Jikubali haikuwa video niliyoipa green light kama wengi walivyofanya.
Adam aliniambia haoni tatizo la rangi hiyo na akaniambia, nakumbuka kabisa alisema ‘the kid is good’. Sikutaka kubisha tena kwakuwa tayari mtu anayejua sana masuala ya video alikuwa ameshasema video iko poa.
Kabla ya hapo, Adam Juma aliwahi kumpa ushauri Nisher kwenye video ya Mama Yeyoo ya G-Nako ft Ben Pol.
“Dude video is ok, stop using that color preset from magic bullet their crushing the black on the picture as a result all the details from the skin tone are gone. Another thing is, use a proper monitor from your edit suite to preview you colours for broadcast, don’t just trust these stupid macbook screens over a simple TV set that everyone views videos from. Yes you have talent, groom it to the direction with knowledge and you will surpass anything,” alishauri Adam.
Nisher alijibu: Many Thanx @Adam Juma … points taken boss… I used HDMI LED Monitors to edit and color grade the video… I didn’t use magic bullet to grade the images but only to flatten them some more… I created my own color palates using AE & Yano Moods… the skin tones are not too visible might be because of YouTube codecs during upload… but thanks for checking it out.” Mafahali hawa waliwasiliana kwa lugha ya fani yao zaidi na kutuacha wengine kapa.
Kwanini Adam Juma ni muongozaji bora wa video kuwahi kutokea Tanzania?
Kama Majani alivyo ‘Godfather of Bongo Flava’ basi Adam ndio ‘Godfather of Bonga Flava music videos’. Adam ndiye aliyebadilisha kabisa muonekano wa video za Tanzania ambazo enzi zile zilikuwa zikikutana na nyundo nzito ya Salama Jabir kwenye Planet Bongo ya EATV. Siwezi kubeza mchango wa video za makampuni kama Benchmark Production iliyotengeneza video ya Zali la Mentali ya Profesa Jay, Mwanachi Videos, 2 Eyez Production iliyofanya video kibao kama Zeze ya TID ft Jay Mo, Royal Production iliyotengeneza video ya Crazy GK ‘Hii Leo ft AY na Mwana FA, Chapakazi Films, Tripod Media na zingine.
Adam Juma
Lakini hakuna ubishi kuwa Adam ndiye aliyeanza kutengeneza video zenye ubora mkubwa na hivyo kufuatwa na wasanii wengi. Mpaka leo hii, sio rahisi kumpata Adam kwa video, yuko busy kila siku. Ndiye aliyeleta mapinduzi ya video za muziki Tanzania. Video zake nyingi ndio zilianza kuchezwa kwenye vituo vikubwa vikiwemo Channel O na MTV Base. Uwezo wa Adam ulifanya achukuliwe pia na wasanii wa nje ya Tanzania kufanya video zao.
Hakuna muongozaji mwingine aliyeweza kufikia kiwango cha Adam. Kama alivyo P-Funk kwenye audio, Adam ndiye muongozaji wa video Tanzania aliyefanya video nyingi zaidi na za maana nchini kuliko muongozaji yeyote. Heshima hiyo haipaswi kuondolewa kwenye historia yake.
Adam hafanyi video za muziki peke yake. Uwezo wake umetumika katika kufanya miradi mikubwa zaidi ya video za muziki. Hufanya matangazo ya biashara pamoja na makala za video ambavyo humpa fedha nyingi zaidi.
Imefika wakati ambao anafikiria kufanya mambo makubwa zaidi kama kufanya movie zenye kiwango kikubwa.
Filamu ya Adam, Protocol iliyopo kwenye maandalizi
Ndio maana alitangaza kuacha kufanya video kibiashara. Ameendelea kufanya hivyo kwa mapenzi yake tu na kwa wasanii wachache.
Kwanini Nisher ni kitu kikubwa kijacho?
Jina la Nisher limekuwa kwa kasi mno kiasi cha kuwazidi hata waongozaji wengi waliokuwepo kabla yake. Kinachomsaidia, ni kule kutumia zaidi ya mitandao ya kijamii kupromote kazi zake. Kwa kufanya hivyo tayari ameshatengeneza fan base, tofauti na waongozaji wengine. Nisher amekuwa celebrity pia, kitu ambacho waongozaji wengine wameshindwa kufanya na hata wengine hawajulikani kwa sura.
Pamoja na kuwa muongozaji wa video, Nisher ni producer wa muziki
Tangu ameanza kufanya video, video zake zimekuwa zikisubiriwa kwa hamu mno. Hii ni kwasababu amekuwa akipromote kazi anazozifanya na sio kuwaachia wasanii wenyewe wafanye hivyo. Waongozaji wengine akiwemo Adam mwenyewe, wamekuwa ni watu wa kufanya video na kuwakabidhi wasanii wenyewe wazipromote. Pengine hicho ni kitu ambacho wenzake wanatakiwa kujifunza kutoka kwake.
Akiwa na muda mfupi tu tangu aanze kufanya video, tayari amefanikiwa kuchezwa kwa video alizoziongoza yeye Channel O ambako huchagua sana video za kucheza. Tangu ameanza, ni rahisi kuona mabadiliko yaliyopo kwenye video zake na jinsi ambavyo anakua haraka. Kutoka kwenye video zenye giza, hadi video zenye muonekano wa kuvutia kama video ya Jordan na Mirror, ‘Bila Wewe’.
Tazama vizuri video zake na namna anavyocheza na camera na kisha kuchanganya picha kiustadi.
Niseme wazi kuwa, uwepo wa Nisher umeleta changamoto kubwa kwa waongozaji wengine wa video nchini. Ushindani huo aliousababisha ulikuwa ukihitajika kwa muda mrefu kwenye sekta hiyo kwakuwa tayari kuna ushindani mkali baina ya wasanii na hata waandaji wa muziki.
Hiki anachokifanya Nisher ambacho kwa wengine kinaweza kuonekana kama kutafuta kiki, kinawafanya waongozaji wengine wakaze zaidi kuthibitisha kuwa pamoja na kwamba hawatajwi, wao pia wanaweza. Matokeo yake ni kuwa, video za hapa hapa nyumbani zinakuwa bora zaidi na kupunguza kasumba iliyojengeka kwa sasa ya wasanii kwenda kufanya video Kenya na Afrika Kusini.
Ushindani huu ni muhimu uwepo.

- Original - from - Bongo5-
No comments: