
Hakuna ubishi kuwa, kwa hiki walichokifanya sasa, na kama macho yetu hayatudanganyi kwa hiki yanayokiona, mapacha hawa wamefanya kufuru. Kama hii inayoonekana ni dhahabu kweli, basi P-Square, hela wanayo.

Kwenye picha nyingine, wanaoonekana wakiwa pamoja kwenye sebule hiyo iliyotawaliwa na kile kinachoonekana kama dhahabu zilizozunguka sofa za kuvutia na Peter ameandika: #2kings…… Work hard,play harder.’
Picha nyingine inamuonesha Peter akiwa peke yake kwenye meza ya chakula, kubwa, iliyojaa vyombo vya thamani vya kuvutia na ameandika: A king in my own world…. #Blessed.”
No comments: