Katika uzinduzi huo uliofanyika katika Maktaba Kuu ya Taifa jijini Dar es salaam ulihudhuriwa na wadau mbalimbali wa elimu, pamoja na rafiki zake Miss Tanzania wa mwaka 2000, Jacqueline Ntuyabaliwe aka ‘K-Lynn, na Nancy Sumari, Miss Tanzania 2005.
Akizungumza na katika uzinduzi huo Faraja Kotta amesema kitabu hicho kinalenga kusaidia wanafunzi kujenga uwezo na maarifa ili kumudu masomo yao.
“Kitabu cha ‘Unaweza’ Mbinu kumi za kumudu masomo yako, kilizaliwa kwasababu nimeona kuna haja ya wanafunzi kuhimili changamoto za uanafunzi na kufanikisha vyema azma ya kwenda shule. Tunajifunza kila siku,kuna wakati tunajua kwamba hapa sasa tunajifunza na kuna wakati hatujui kwamba tunajifunza.Ni muhimu kujenga misingi hii ya kujifunza mapema,” alisema Faraja.
Pia Faraja amewapongeza wanafunzi wote wanaotambua umuhimu wa kutumia maktaba,akisema ni mfano wa kuigwa.
Aidha Faraja ametoa wito kwa watu mbalimbali wenye mapenzi mema na elimu kuhifadhi upatikanaji wa kitabu cha ‘Unaweza’ kwenye maktaba nyingine za mikoa na wilaya.Huku akisema asilimia 50 ya mauzo ya kitabu cha ‘Unaweza’ yataenda Chuo cha Ualimu cha Korogwe,hususan chumba cha Teknohama kwa ajili ya kuboresha upatikanaji wa elimu wa teknolojia.
Nancy Sumari
Wadau walioudhuria uzinduzi huo
No comments: