KIHARUSI au kwa Kiingereza Stroke ni kitendo cha baadhi ya viungo vya mwili kuwa na ganzi au kutojiweza kufanya kazi zake za kawaida.Kuna aina mbili za kiharusi lakini kabla ya kuchambua hayo tuangalie, ni nini kinasababisha mtu kukumbwa na ugonjwa huo?Mtu anaweza kupata dalili za ugonjwa huu wa kiharusi na baada ya dakika chake zikaisha.
Kiharusi kinampata binadamu baada ya eneo la ubongo kukosa damu kwa saa 24 ama zaidi au kunapotokea kizuizi cha damu au mishipa ya damu kushindwa kusafirisha damu au mshipa huo unapopasuka.
Kiharusi kimegawanyika katika aina kuu mbili kulingana na jinsi kinavyotokea, kwanza ni:
Kiharusi cha kukosa hewa kwenye ubongo kitaalamu huitwa Ischemic stroke. (Ischemic ni neno la Kigiriki lenye maana ya kuzuia damu).Aina hii ya kiharusi hutokea iwapo usambazaji wa damu katika sehemu ya ubongo hupungua na kusababisha tishu za ubongo za eneo lililoathirika kushindwa kufanya kazi zake vizuri.Hiki hutokea baada ya mshipa wa ateri kuziba kutokana na kuganda kwa damu, hali ambayo inasababisha damu isisafiri vyema na kuelekea kwenye ubongo.Hali hiyo pia hufanya damu iliyoganda kuziba mishipa midogo ndani ya ubongo kitaalamu huitwa Cerebral thrombosis au kipande cha damu kumeguka na kwenda kuziba mshipa wa damu kwenye ubongo kitaalamu huitwa Cerebral embolism.Lakini tatizo hili linaweza kutokea pale damu inapoganda sehemu nyingine ya mwili na kusafiri hadi kwenye mishipa ya ateri, hivyo kusababisha damu kwenda kwenye ubongo kukwama.Hata hivyo, tatizo hili linaweza kusababisha kitu kinachoitwa Lacunar stroke, yaani vimirija vidogovidogo sana vya damu vilivyopo ndani ya ubongo, vinaziba.Hapo sasa binadamu huwa anakumbwa na kiharusi kinachojulikana kitaalamu kama Lacunar stroke japokuwa mara nyingi hii haiwaletei sana shida wagonjwa.KIHARUSI CHA HAEMORRHAGE
Baada ya kufafanua kiharusi kinachoitwa Ischaemia ambacho ndani yake tukaelezea pia kile kinachoitwa Lacunar stroke, sasa tuelezee aina ya kiharusi kiitwacho Haemorrhage.Aina hii ya kiharusi mrija wa damu karibu ama kwenye ubongo hupata mpasuko, hivyo kusababisha damu kuvuja na kitendo hicho ndicho kitaalamu huitwa Haemorrhage.Kinachotokea ni kwamba damu inayovuja hukandamiza ubongo na kuuharibu, ubongo ni moja ya kiungo laini sana mwilini.
Kiharusi kinampata binadamu baada ya eneo la ubongo kukosa damu kwa saa 24 ama zaidi au kunapotokea kizuizi cha damu au mishipa ya damu kushindwa kusafirisha damu au mshipa huo unapopasuka.
Kiharusi cha kukosa hewa kwenye ubongo kitaalamu huitwa Ischemic stroke. (Ischemic ni neno la Kigiriki lenye maana ya kuzuia damu).
Baada ya kufafanua kiharusi kinachoitwa Ischaemia ambacho ndani yake tukaelezea pia kile kinachoitwa Lacunar stroke, sasa tuelezee aina ya kiharusi kiitwacho Haemorrhage.
No comments: