Muigizaji Mkongwe wa filamu na mshindi wa tuzo za Oscar, Philip Seymour Hoffman amefariki dunia akiwa nyumbani kwake jijini New York akiwa na miaka 46.
Mwili wake ulipatikana baada ya rafiki yake kupiga simu ya dharura. Polisi wamesema muigizaji huyo atakuwa amefariki kutokana na kuzidisha matumizi ya madawa ya kulevya.
Philip Seymour Hoffman
Mwili wa Hoffman ulipatikana ukiwa na bomba la sindano lililokuwa limeng’ang’ania kwenyr mkono wake wa kushoto na kwmaba kulikuwa na madawa ya kulevya aina ya heroin kwenye bahasha kadhaa. Polisi wamesema muigizaji huyo alikutwa akiwa na nguo zake na akiwa amelala sakafuni kwenye bafuni.
Muigizaji huyo amewahi kuigiza filamu kibao ikiwemo Mission Impossible III na mfululizo wa filamu za Hunger Games.
Muigizaji huyo amewahi kuigiza filamu kibao ikiwemo Mission Impossible III na mfululizo wa filamu za Hunger Games.
No comments: