» » » » Jux azungumzia jinsi muziki wa Bongo Flava unavyochukuliwa nchini China na wasanii wanaofanya vizuri

ember wa kundi la Wakacha na mwimbaji wa ‘Uzuri Wako’, Jux ambaye amekaa nchini China kimasomo kwa muda mrefu, ameizungumzia jinsi ambavyo muziki wa Bongo Flava unavyochukuliwa nchini humo.

Jux ameiambia tovuti ya Times fm kuwa wachina ni wazalendo sana kwa muziki wao wa nyumbani na kwamba hawaweki mwanya kwa miziki mingine ya nje kuchukua nafasi ama hata kutambulika zaidi nchini humo hivyo hata muziki wa Afrika haupewi nafasi kwenye club za wazawa.


Jux

“Kwa kule siwezi kusema uongo, wachina kama wachina club zao za kule waga hazipigwi kabisa nyimbo za kiafrika. Nyimbo zote unazozifahamu za Afrika waga hazipegwi. Na hata za Kimarekani ni baadhi, yaani zile zinazokuwa billboard. Wana club zao kubwa kubwa kama hizi club zetu labda Billicanas na nyingine kubwa kubwa, kwa wao kule wachina mji niliokuwepo mimi hawapigagi nyimbo za Afrika.” Amesema Jux.

Ingawa nyimbo za Afrika hazipigwi kwenye club kubwa huko China, zipo sehemu ambazo ukiwa na kiu ya nyimbo za kibongo ama za kiafrika inabidi uelekee na huko mtakutana na ndugu zako wa Afrika na Tanzania mcheze kikwenu.

“Sehemu ambazo utakuta nyimbo za Kiafrika ni zile club za Kiafrika, sehemu ambazo wanaenda wanigeria, wanaenda waghana wanaenda watanzania wanapiga nyimbo za Kiafrika. Na nyimbo zinazopendwa sana ni nyimbo za Kinigeria.” Ameeleza Jux.

Lakini nyimbo gani zinahit hata kwenye hizo club za kiafrika wanakoenda watanzania?

“Ni sawa sawa na huku, nyimbo ambayo itahit huku na kule inafanya vizuri. Kama hivyo nyimbo za Diamond, nyimbo za hao wanigeria, nyimbo za akina Rich. Nyimbo zote za kibongo zinazofanya club vizuri huku na kule ni the same. Kwa sababu wanaoenda kwanza club hizo katika asilimia 100, asilimia 90 ni waafrika. Wachina ni wachache, wanaweza kuwa labda ni wafanyakazi labda wa mule club. Kwa sababu walishajiwekea system ya kila kitu hata wasanii wao wanawapa kipaumbele zaidi.” Ameongeza mwimbaji huyo wa Nitasubiri.

Jux ameeleza kuwa kwa jinsi wachina wanavyowapenda wasanii wa nyumbani, wengi hawawafahamu hata wasanii wakubwa wanaofanya vizuri Marekani kiasi kwamba alikutana na B.OB kwenye shopping mall na hakuna mchina aliyeonesha kumfahamu tofauti na ambavyo labda angekuwa Tanzania.

Amedai inawezekana msanii kama R. Kelly akafunikwa kabisa na msanii wa pale China katika tamasha lake kwa kuwa msanii maarufu wa China anaweza kumzidi umaarufu R.Kelly kwenye mipaka ya mji aliokuwepo Jux na ukizingatia kuwa karibu robo ya idadi ya watu duniani wako China.

“Yaani huwezi kukuta labda eti unapita barabarani halafu unakuta labda kuna sehemu wimbo wa P-Square unapigwa. Wale wana wasanii wao wa nyumbani wanaowapenda zaidi.” Jux amesisitiza.

Tunaweza kusema ni kama ambavyo miziki ya Kichina haifanyi vizuri katika club za Bongo, japo Gangnam Style ya mkorea PSY jirani zao ni hadithi nyingine Tanzania na duniani kwa ujumla.


Chanzo:TimesNews

Tunaomba Maoni yako Hapa :

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply