Najua wengi mtakuwa mnakumbuka kila msikiapo neno kerewa ,kukumbuka track mpya ya shetta inayo-make headlines sana hapa town hivi sasa akiwa amemshirikisha Diamond Platnumz,ila je unajua maana halisi ya neno hilo?..
Kwa Definition kutoka Google haswa linavyotumika neno hilo huko Nchi za west Africa maana yake halisi ni uasherati a.k.a ”michepuko” au hali yakumsaliti mwenza wako,
Neno hili linatupeleka hadi west africa ambapo ndiko hutumika sana na kuna baadhi ya nyimbo zilishawahi kutoka zikiwa zinatumia title kama hiyokerewa ,ila moja ya nyimbo ambayo iliwahi kutoka huko nchini Nigeria na kundi moja linaloitwa Zulezoo ilishia kufungiwa na serikali ya nchi hiyo mwezi march mwaka 2006,kutokana na kinachosemekana kuwa nyimbo hiyo ilikuwa imejaana mashairi makali yaliyotumika kwenye wimbo huo yanayochochea uasherati katika jamii na kuenda kinyume na tamaduni za ki-Africa.
Nyimbo hiyo iliyokuwa inaelezea tu jinsi mke ambae alikuwa si muaminifu kwa mume wake,akimsaliti mume wake na mwanamme mwingine wakati mume wake akiwa safarini na si vinginevyo kama board yao ilivyoelewa na kupelekea kufungiwa.
Kwa hapa home Tzii ni moja ya nyimbo ambayo imeweza kupata umaaarufu mkubwa na kuendelea kupata airtime yakutosha kutoka kwenye media mbalimbali za hapa Bongo,hii yote ni kutokana na ubora wa kazi nzuri za wasanii walioufanya wimbo huo na kufanya wimbo huo kuwa requested mara nyingi na fans mbalimbali wa muziki wa Bongo Fleva siku hadi siku…
Via:NewsShare
No comments: