» » » » Jay Z na Beyonce kuwapatia Kanye na Kim zawadi hii nono, ila wao hawatahudhuria harusi hiyo

Ili kumpoza Kanye West na kulinda urafiki wao usivunjike kwakuwa hawatahudhuria harusi yake na Kim Kardashian, Jay Z na Beyonce watawapa wapenzi hao zawadi nzuri.




Jay Z na mkewe Bey wamegoma kuhudhuria harusi hiyo itakayofanyika May 24 jijini Paris, Ufaransa kwakuwa hawataki waonekane kwenye show ya Keeping Up With The Kardashians. Chanzo kimoja kimeliambia gazeti la The Sun kuwa Hov angeweza kuhudhuria kama ingekuwa sio harusi ya wazi hivyo.

Hata hivyo, pamoja na kwamba Jay na Beyonce hawatakuwepo, rapper huyo atawalipia gharama za kukodi meli binafsi ya £100,000 ili waitumie kwenye fungate aka honeymoon. Jay pia amepanga kumwandalia Kanye party ya kufa mtu kwenye club yake ya New York, 40/40.

Tunaomba Maoni yako Hapa :

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply