» » KTMA 2014: Mchakato wa kupiga kura kuelekea kikomo

Kampuni ya Bia Tanzania inayotengeneza kinywaji cha Kilimanjaro, leo hii imekutana na waandishi wa habari kuzungumzia mwenendo wa mchakato wa kuwapata washindi wa tuzo za muziki Tanzania, Kilimanjaro Tanzania Music Awards 2014, mchakato ambao unaendelea kwa mwezi huu mzima kwa njia ya watanzania kupiga kura.



Meneja wa Kinywaji cha Kilimanjaro, Bwana George Kavishe amewataka watanzania kuendelea kupiga kura kwa wingi katika siku 6 zilizobakia, ili kukamilisha asilimia 70 walizopewa kuchagua ni msanii gani anayestahili kuchukua tuzo kwa mwaka huu.
Bwana Kavishe amesema kuwa, asilimia 30 zilizobaki katika kuamua washindi, zitaamuliwa na timu ya majaji itakayoundwa na wadau wa chati za muziki na wataalam, wakizingatia vigezo ambavyo vitawekwa wazi na BASATA hivi karibuni.

Tunaomba Maoni yako Hapa :

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply