Mtandao wa Naija Gists umeripoti kuwa kwa mujibu wa chanzo, inadaiwa kuwa kumekuwa na kutoelewana baina ya kaka mkubwa wa mapacha hao Jude Okoye na mke wa mdogo wake Peter Okoye aitwaye Lola Omotayo, kitu kilichopelekea Jude kutohudhuria harusi yao mwaka jana.
Kama unakumbuka Jude hakuhudhuria harusi ya Peter na Lola mwaka jana, lakini alihudhuria ya Paul na Anita mwaka huu kitu kinachowafanya watu waamini kuwa kuna tatizo kubwa baina yao.
Chanzo hicho kimesema inadaiwa kuwa ugomvi huo unaomhusu Lola umesababisha Peter na Paul kugombana wakati wako kwenye rehearsle Jumatano wiki hii, mpaka walipoachanishwa na dancers wao.
“After over 10 years of hard work, it’s over. (I) Am done.” ikiaminika kuwa alimaanisha amejiondoa kuli-manage kundi hilo japo kuwa yeye mwenyewe hakufafanua alichomaanisha katika maneno hayo machache.
Jude ndiye amekuwa akiwa-manage kwa miaka yote na kuproduce hits zao paomoja na kudirect idadi kubwa ya video zao zilizofanya vizuri.
Lakini kuna baadhi ya watu nchini Nigeria wamedai kubwa kuna uwezekano kuwa ugomvi ‘hewa’ unaoendelea na kuripotiwa katika vyombo vya habari ukawa ni ‘hype’ ya kuandaa ‘kiki’ ya album yao mpya.
No comments: