» » » Pastor Myamba kufunga ndoa August 2 2014 Zanzibar

Msanii wa filamu, Emmanuel Myamba aka Pastor Myamba anatarajia kufunga ndoa na mwanadada Trakseda Kasela, itayofanyikia August 2 huko visiwani Zanzibar.



Akizungumza na Bongo61kwa kupitia simu  siku ya jana Pastor Myamba amesema kuwa huu ndiy wakati wake ambao ameamua kufunga ndoa na kukaa na mke wake pamoja.

“Mwezi wa nane tarehe mbili Mungu akinijalia nitakuwa naoa, mke wangu ni wa hapa hapa Dar es Salaam lakini sio msanii, sipendi kuoa wasanii bwana, wasanii mambo mengi,” amesema. “Mpaka sasa hivi ninatoa tu taarifa nadhani harusi yangu haitafanyikia kanisani na itafanyikia kwenye garden huko Zanzibar. Mpaka sasa hivi bado nipo kwenye maandalizi ya mwisho, kwahiyo msishangae siku ya mwisho nabadili baada ya kwenda kufungia Zanzibar nikafanyia hapahapa. Lakini kila kitu kipo sawa kwamba natarajia kuoa sasa na kuishi pamoja na mke wangu, ninayetarajia kumuoa anaitwa Trakseda Kasela.”

Tunaomba Maoni yako Hapa :

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply