Habari kwa Ufupi :

» » Pokello avishwa pete ya uchumba na Elikem wa BBA ni katika tuzo za ‘Ghana Music Awards’ Jumamosi

Wapenzi walioanzia mapenzi yao katika jumba  la BBAkati ya Mghana Elikem na Pokello wa Zimbabwe imeingia katika hatua ya juu baada ya Elikem kumvisha pete ya uchumba wakati wa show ya Tuzo za Ghana jumamosi iliyopita huko Accra, Ghana.




Tukio hilo special kwa wawili lilitokea walipoitwa jukwaani kutamtangaza mshindi wa Tuzo ya ‘Best Collabo of 2014’, ndipo Elikem aliu-surprise ukumbi mzima baada ya kupiga goti na kumuuliza Pokello lile swali adimu na muhimu, ‘Will you marry me’, na jibu la ‘Yes’ kutoka kwa Pokello liliamsha shangwe ukumbini hapo.

Wapenzi hao ambao walipewa jina moja la Polikem ilizaliwa wakati wa msimu wa nane wa reality show ya Big Brother Africa mwaka jana.

Dada yetu Feza na shemeji O’neal nyinyi mtatu-surprise lini?

Photo Credit: Bella Naija

Tunaomba Maoni yako Hapa :

«
Next
Video: Adam Mchomvu a.k.a Baba Jonii - Au Sio (Official Videos)
»
Previous
Magari 30 ya Paul Walker yawekwa mnadani, jina lake kutotumika katika uuzaji

No comments:

Leave a Reply