Habari kwa Ufupi :

» » » Breaking News: Mzee Small Afariki Dunia

Muigizaji mkongwe aliyetamba miaka mingi kwa filamu za vichekesho Said Ngamba maarufu kwa jina la Mzee Small amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika hospitali ya taifa ya Muhimbili.

Habari hizi za kusikitisha zimeripotiwa na chanzo cha kuaminika ambacho kimeeleza kuwa alizidiwa na ugonjwa wa presha uliopelekea kifo chake.

Muigizaji huyo amekuwa akisumbuliwa na magonjwa kwa muda mrefu hali iliyompelekea kulemaa viungo hususani mkono wake.

Taarifa hizi ni mwiba mwingine kwa tasnia ya filamu nchini ikiwa ni wiki moja imepita tangu marehemu George Tyson afariki kwa ajali ya gari.
Bongo61 Tunawapa pole wafiwa wote na Tasnia ya Filamu kwa ujumla 'Mungu ailaze pema roho ya Mzee Small. Amina!

Tunaomba Maoni yako Hapa :

«
Next
Magazetini leo Jumapili ya Tarehe 08/6/2014
»
Previous
Haya ndio Matokeo ya Diamond kwenye MAMA Awards

No comments:

Leave a Reply