Kwa mujibu wa mtandao wa The Hollywood Reporter, staa huyo wa Disney Channel ataigiza kama marehemu Aaliyah kwenye filamu iitwayo Aaliyah: Princess of R&B.
Filamu hiyo imebase kwenye kitabu cha historia ya Aaliyah kilichoandikwa na Christopher Farley, Aaliyah: More Than a Woman.
Filamu hiyo inatayarishwa na Aaliyah Productions Inc. huku Howard Braunstein (The Informant!) na Debra Martin Chase (The Princess Diaries) wakiwa watayarishaji wakuu. Bradley Walsh (Turn the Beat Around) ataongoza filamu hiyo ambapo script yake imeandikwa na Michael Elliot (Brown Sugar).
“She’s been an inspiration and influence in my whole career, her talent still shines brighter then ever, all I wanna do is honor her,” Zendaya aliandika kwenye Twitter. “Show how much she accomplished in only 22 years….she’s beautiful inside and there will never be another Aaliyah, I just hope to share her beautiful story, and make her proud up in heaven.
Lifetime pia inaanda filamu ya maisha ya Whitney Houston iliyoongozwa Angela Bassett na starring akiwa Yaya DaCosta.
No comments: