Rapper Fid Q amesema ni mapema sana kuzungumzia masuala ya ndoa na mpenzi wake kutoka Jamhuri ya Czech aliyejifungua mtoto wa kike aitwaye Fidelie Ijumaa hii.
Fid Q ameiambia 255 ya kipindi cha XXL, Clouds FM kuwa kuna mambo mazuri mengi yanakuja kati yao.
“Huyu ni mtoto wangu wa kwanza wa kike na kwa haraka haraka mimi nina watoto wawili wa kiume. Huyu mama yake alikuwa girlfriend wangu wa muda mrefu sana, yale masuala ya ndoa na nini nisingependa kuyaongelea leo, itakuwa umeyaharakisha sana lakini natarajia mambo mengi mazuri. Pia japokuwa nimetingwa na shughuli nyingi hapa nchini lakini nafanya mpango wa kukutana naye,” alisema Fid Q.
No comments: