Ukipata mchumba hasa mmachame wanafamilia wanakuwa wagumu kubariki mahusiano yenu.Hii imetokana na baadhi ya jamii kutendwa baada ya kuoa wachaga.Lakini naamini kuna baadhi ya dada zangu wa kichaga ni wema kabisa na wanamtegemea Mungu na upendo wao unaweza kufuta mabaya yaliyojengeka ktk jamii zetu kwa vizazi vilivyopita.
Hapo awali wanaume wa kikurya walikuwa wanaogopwa na mabinti wengi sana kwa sababu ya kutoa kichapo lakini siku hizi baada ya jamii kuona baadhi ya wadada wameolewa na watu hao na wamepewa mapenzi ya dhati jamii imewakubali.Leo hii ukipata mchumba wa kikurya halafu ukampeleka nyumbani anakubalika.
Hivyo dada zangu jisafisheni kufuta mfumo dume uliojengeka ktk jamii pia mnaweza kutujuza tatizo liko wapi mpaka jamii inaogopa?
No comments: