» » Watoto wa Nelson Mandela kuhudhuria tuzo za Oscars

Watoto wa kike wa Nelson Mandela, Zindziswa na Zenani watahudhuria tuzo za Oscars 2014, zitakazotolewa weekend ijayo jijini Los Angeles, Marekani. Wawili hao walialikwa na the Academy of Motion Picture Arts and Sciences ili wawashuhudie wanamuziki wa U2 wakiimba wimbo uliotajwa kwenye tuzo hizo, Ordinary Love.




Wimbo huo umetumika kwenye filamu ya Mandela: Long Walk To Freedom, iliyoangalia maisha ya kiongozi huyo wa zamani wa Afrika Kusini aliyefariki mwishoni mwa mwaka jana. Filamu hiyo imeigizwa na Idris Elba kama Mandela.

Baada ya kupata mwaliko huo, Zindziswa na Zenani walitoa maelezo kwa kusema kuwa wameufurahia kwakuwa baba yao alikuwa akipenda kutazama movie. “[Ordinary Love] was inspired by the beautiful letters that my father and mother exchanged while he was imprisoned at Robben Island,” maelezo hayo yalisema.

Zenani na Zindziswa (Zindzi) ni watoto wa mwisho kati ya watoto sita wa Mandela kutoka kwa mke wake wa Winnie Madikizela-Mandela.

Tuzo za Oscars zitatolewa Jumapili. March 2 na zitarushwa live.

Source:Bongo5

Tunaomba Maoni yako Hapa :

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply