» » » VODACOM NA NOKIA ZAZINDUA NOKIA LUMIA 820 NA 920


003 8f492
Dar es Salaam...Watuamiaji wa simu za mkononi kuanzia sasa wataanza kunufaika na simu za Nokia Lumia 920 na Lumia 820 zinazokidhi matakwa ya mtumiaji kulingana na teknolojia ya sasa, baada ya Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom nchini kwa kushirikiana na Nokia kuzitambulisha rasmi sokoni.
Simu hizo ambazo zina uwezo wa kuhimili kimatumizi masafa ya teknolojia ya kiwango cha juu yaani 'Long Term Evolution' LTE, zimezinduliwa Dar es Salaam, ikiwa ni siku chache baada ya Vodacom kukamilisha mchakato wa ufungaji minara yake ya 3G nchi nzima na ile ya 4G kwa jiji la Dar es Salaam.
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi huo, Mkuu wa Kitengo cha Vifaa vya Mawasiliano na Wateja wa Vodacom, Mgopelinyi Kiwanga, alisema kampuni yake inaona fahari na umuhimu kuwaleta karibu wateja wa simu hizo bora (smartphones) katika soko la Tanzania.

"Simu hizi zina uwezo wa kipekee kukidhi mahitaji halisi ya teknolojia ya kiwango cha juu kabisa, ikizingatiwa ubora wake katika kila kifurushi cha huduma yake, mwonekano mzuri wa filamu na picha, haiunganishwi na waya wowote, udadavuaji rahisi wa vifurushi ikiwemo Intaneti, Facebook, Youtube, Twitter, Wikipedia na ina kadi ya kumbukumbu yenye uwezo wa GB 32 na 1GB RAM," alisema Kiwanga.
Aliongeza kuwa kitu kingine kinachokufanya uitambue kwa urahisi Nokia Lumia 920 ni rangi zake ikiwemo manjano, nyekundu na nyeusi wakati Nokia Lumia 820 ina rangi nyekundu, manjano, kijivu, zambarau, nyeusi, nyeupe na sayani
Kwa upande wake, Meneja Masoko wa Nokia Afrika Mashariki, Ellen Lupilli, alisema uwezo wa simu hizo ukilinganisha na smartphones nyingine ina mwonekano safi wa filamu, mafaili na picha, na kutokana na ubora wa lenzi yake unaweza kuchukua picha bila ya kutumia flash usiku na mchana.
Kwa mujibu wa Lupilli, wateja wanaweza kudadavua programu na michezo mbalimbali kama Fifa 12, Tertis na Need for Speed.
"Nokia Lumia 920 na 820 zina vitu vingi vizuri na rahisi kutumia, kiasi kwamba zitawavutia watumiaji wengi kuzinunua," alisema na kuongeza "simu hizo ziko sokoni tayari na unaweza kupata kwenye maduka ya Vodacom nay a Nokia nchini,huku gharama za Lumia 920 ni Sh 1,154,999 na ile ya Lumia 820 inauzwa kwa Sh 809,999," alisema Lupilli.

Tunaomba Maoni yako Hapa :

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply