Na Frank John – Maelezo
Watumishi wa umma wametakiwa kuwa mfano wa kuigwa katika kutekeleza majukumu yao kwa mujibu wa taaluma zao hasa katika kitengo cha manunuzi ili sekta binafsi ziweze kujifunza kutoka kwao. Wito huo umetolewa hivi karibuni na Kamishna wa Idara ya Manunuzi ya Umma kutoka wizara ya Fedha Dk. Fredrick Mwakibinga katika kongamano la kujadili rasimu ya sera ya manunuzi lililofanyika katika ukumbi wa
mikutano wa kimataifa wa JB uliopo jijini Dar es Salaam.
Dk Mwakibinga pia aliwataka Maafisa ugavi, wananchi na wadau mbalimbali kutoa maoni yao juu ya rasimu ya Sera ya manunuzi ya Umma ili waweze kufanikisha zoezi la mchakato wa uundwaji wa sera hiyo.
Alisema kuwa kupatikana kwa sera nzuri na ya kisasa ya manunuzi ya umma ambayo ni muongozo wa Serikali katika sekta hiyo, kutaisaidia Serikali kutimiza nia na malengo ya kuwaletea wananchi maendeleo ya kweli.
“Tunayo mambo mengi ya kuangalia kama Serikali ili kuboresha sekta hii, ikiwa ni pamoja na kuangalia miundo ya Idara za ugavi, idadi ya watumishi na kuwajengea uwezo wagavi ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa weledi zaidi”, alisema Dk. Mwakibinga.
No comments: