Home
»
celebrity News
»
celebrity Photos
»
Jose Chameleone
»
News
» JOSE CHAMELEON AFUNIKA VIBAYA KATIKA SHOO YAKE YA BADILISHA ILIYOFANYIKA UGANDA [PICHA]
Hitmaker wa Valu Valu, Jose Chameleone, jana ameweka historia nchini Uganda kwa kupiga show ya kihistoria, Badilisha Live. Show hiyo iliyofanyika kwenye viwanja vya Kyadondo Rugby Club na kuhudhuriwa na takriban watu 20,000.
Mzazi Willy Tuva (kushoto) alikuwepo kushuhudia historia ikiandikwa
Redsun
Ili kupata picha halisi ya jinsi concert hiyo ilivyokuwa kubwa na yenye mafanikio, tumemtafuta mtangazaji maarufu wa Kenya Mzazi Willy M. Tuva anayetangaza kipindi cha Mambo Mseto cha Radio Citizen na Mseto East Africa cha Citizen TV aliyekuwa shuhuda kwenye viwanja hivyo kutuelezea. Na hivi ndivyo alivyosimulia:
Chameleone ni msanii mkubwa sana Afrika Mashariki na waganda wanamkubali sana. I observed a number of things ambazo Ningependa watu wajue. Chameleone amejipanga vilivyo kwenye maandalizi ya show na performance. Alitawala jukwaa kwa masaa mengi bila kuchosha watu. Aliimba na band.
Jose Chameleone na mwanae
Mke wa Chameleone (Daniella) kulia akiwa na shoga zake kumshuhudia mumewe akifanya yake
Redsun na Profesa Jay wakimshuhudia Dokta
Mzazi Tuva kwenye Twitter aliandika: A mzungu from Norway on stage singing @JChameleone’s #Valuvalu at the #Badilisha concert. Celebrating East African Music
Wasanii waalikwa Profesa J na Redsan walipanda kuimba naye nyimbo mbili tatu na muda wote Chameleone alikuwa jukwaani. Alishtua watu pale alipompandisha mtoto wake jukwaani na akapiga gita vizuri sana wakiimba pamoja.
Chameleone alikuwa na umati mkubwa sana.Kikubwa ni kuwa lugha ya Kiswahili inafaa itukuzwe. Msanii anayeimba Kiswahili anakubalika zaidi kuliko anayeiga tamaduni za Magharibi. Chameleone ni mfano mzuri. Anakubalika kwao na amepenya Kenya na Tanzania. Kwanini? Sababu anaunganisha Uganda na Afrika Mashariki.
Jiulize mbona Bobby Wine na Bebe Cool hawajapenya zaidi nje ya Uganda? Jibu unalo.. Niliwauliza baadhi ya watu wakasema hata kama hawaelewi vizuri (Kiswahili) wanapenda muziki wake na melody zake. Pia anawafanya waganda waelewe Kiswahili. Badilisha ndio wimbo mkubwa zaidi Uganda.�
Baada ya show hiyo Chameleone ameandika kupitia ukurasa wake wa Facebook:
Thank you for making this a remarkable date on my music career calendar. we made history as a team! Badilisha live 26th April 2013…….2014 here I come! Leone Island tugende tukole!
PICHA ZOOTE KUTOKA JOSE CHAMELEON FACEBOOK FAN PAGE
Tunaomba Maoni yako Hapa :
Category: celebrity News celebrity Photos Jose Chameleone News
Related Posts
Picha: Tiffah ni Photocopy ya Baba yake Diamond Platnumz
Tiffah, mtoto wa Diamond Platnumz aliyezaa na mpenzi wake wa Uganda, Zari the Bosslady ni kama photo...Read more »
25Sep2015Fid Q amzunguzia mama wa mtoto wake Fidelie
Rapper Fid Q amesema ni mapema sana kuzungumzia masuala ya ndoa na mpenzi wake kutoka Jamhuri ya Cze...Read more »
26Sep2015Kajala Ammwagia Zari Minoti!
KIMENUKA tena! Katika kile kinachoonekana kama ni kejeli kwa shosti wake wa zamani, ambaye sasa pic...Read more »
25Sep2015Je Umeshawahi Kujiuliza Kama Kuna Ugomvi Wowote Kati ya Lulu Michael na Wema Sepetu...? Lulu Afunguka Haya
KAMA unafikiri kuna ugonvi kati ya waigizaji maarufu nchini, Elizabeth Michael, ‘Lulu’ na Wema Sepet...Read more »
25Sep2015Dk. Cheni Afunguka Kumuoa Lulu!
Tangu wakati ule msanii maarufu wa filamu, Mahsein Awadh ‘Dk. Cheni’ aamue kupambana kumsaidia Eliza...Read more »
25Sep2015Mama wa Diamond Aongelea Kuhusu Mjukuu wake Kuwa si Mtoto wa Diamond
Weekend iliyopita mtoto wa Diamond na Zari aitwaye Tiffah alitimiza siku 40 na sura yake kuonyeshwa ...Read more »
25Sep2015
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments: