» » » » KIDOTI TIME IKIWA CHINI YA OWNER WAKE JOKATE MWEGELO WAKO SONGEA KUVUMBUA VIPAJI VYA WANAFUNZI




Mrembo, mtangazaji na mjasiriamali nchini Jokate Mwegelo weekend hii amekuwa mgeni rasmi kwenye mashindano ya UMISSETA 2013 ngazi ya wilaya katika halmashauri ya Songea mkoani Ruvuma.


Jokate alikuwa mgeni rasmi kupitia kampeni yake ya Kidoti Time yenye lengo la kusaidia kuibua vipaji vya wanafunzi pamoja na kuwainspire. “Naamini kila mtu Mungu aliyemuumba amempa kipawa chake ila tatizo ni namna ya kukiibua,” alisema Jokate wakati wa ufunguzi huo.



“Elimu ni jambo la msingi sana,nimeona ni vyema tutafute mbinu za kuwahamasisha wanafunzi kupenda kuja shule kwa kutumia program ya Kidoti.

Kidoti time ni program ambayo itafanyika mashuleni kuanzia term(muhula) ijayo ya masomo ikilenga kuvumbua vipaji mbalimbali walivyonavyo wanafunzi, naamini kuna wanafunzi wana uwezo wa kuimba,kuchora,ubunifu,kucheza,kuigiza na vipaji vingine vingi.

Uwezo huu wa vipaji vyao ukiibuliwa na kuendelezwa unaweza kuwafanya siku moja wakatambulika na kutoa mchango mkubwa kwa jamii wa kifikra na kimaendeleo kupitia vipaji vyao”.




Mashindano hayo yenye kauli mbiu ya Jifunze,Cheza,Shinda , yanazikutanisha cluster 5 zinazounda halmashauri ya Songea.

Tunaomba Maoni yako Hapa :

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply